Akitumia mitandao yake ya kijamii, sosholaiti huyo alisema rafiki yake alimpeleka kanisani Jumapili katika jumba la King's House huko London.
Vera Sidika alisema mwaka ulipoanza, alipendekeza kuunda mshikamano wa karibu na Mungu, lakini, kila wakati alipojiahidi kuhudhuria moja, alijisahau au kushikana. Kwa zaidi ya miaka 10, Vera Sidika alifurahi siku ya Jumapili baada ya rafiki yake kumpeleka kanisani huko London.
Sosholaiti huyo alisema kuwa mahubiri yalikuwa mazuri na alitarajia kufurahia uwepo wa Mungu.
“Jumapili hii iliyopita ilikuwa mara yangu ya kwanza kanisani kwa zaidi ya miaka 10 shukrani kwa BFF wangu @dyna_muthoni. Ilikuwa azimio yangu ya mwaka mpya lakini shetani aliijaribu kwa miezi 10. Kila mara ‘nilisema nitaanza Jumapili hii’ haikuwahi kutokea. King’s house ni kanisa nzuri kweli,” aliandika.
Mapema mwaka huu Vera Sidika alisema kwamba anataka kuboresha uhusiano wake na Mungu. Sidika kupitia instastory zake, alisema kwamba angependa kuanza kuhudhuria ibada kanisani katika kipindi cha mwaka huu, akisema kwamba hiyo ndio njia pekee ya kuimarisha Zaidi uhusiano wake na Muumba wake.
Kwa namna hiyo, Sidika aliwaomba mashabiki wake katika mtandao huo kumpa ushauri wa ni kanisa lipi zuri la kufanya mahudhurio ya ibada, akisema kwamba licha ya kuwa na uhusiano mzuri na Mungu, kwa muda mrefu sasa hajawai tia guu lake katika malango ya kanisa.
Mama huyo wa watoto wawili alisema kwamba aliwahi jaribu kufanya hivyo kwa wakati mmoja lakini akapata kila mtu macho yanamtoka pima pindi tu wanapomuona kanisani, jambo lililomchochea kujivuta nyuma katika suala zima la kwenda kanisani.
“Mwaka huu wa 2024 ninataka kujenga uhusiano mwema na Mungu, sijawahi kuenda kanisani kwa muda sasa, mimi ni muumini, namuomba Mungu na kufanya upande wangu kama Mkristo.
Lakini inniwia vigumu kwenda kanisani. Watu wananiangalia sana. Kunaye mmoja wenu ambaye anajua kanisa zuri ambalo sitoweza kusumbuliwa na kuangaliwa, tafadhali pendekeza moja,” Vera Sidika aliomba.
Lakini pia alisisitiza kwamba asingependa kupendekezewa kanisa katika sehemu yoyote ile akisisitiza kwamba angependa kuhudhuria kanisa katika maeneo ya Kifahari ya Karen.
“Ikiwezekana iwe Karen,” Sidika aliongeza.