Akitumia YouTube channel yake, Milly Chebby amefichua kwamba tangu Januari mpaka Oktoba mwaka huu, ameajiri yaya 19.
“Tangu the last nanny wa Milla atoke, I know I updated you guys on my Instagram, nimegonga 19. Wanakuja wawili, wanaenda. Wengine wawili wanaenda,” Chebby anasema kuwa kitambo alikuwa na hofu yaya walipokuwa wanaenda lakini sasa amekuwa mgumu na haogopi yaya akiamua kwenda akisema maisha itaendelea.
“Kitambo nilikuwa naogopa na kuwaza ooh sasa Milla nitafanya? ghai sasa shule kesho. Lakini sahizi mimi nilijiambia hata kikiumana zaidi, Milla kaa kiti ya nyuma, maisha inaendelea,” Milly pia amesema kwa sasa ana yaya wawili, mmoja akiwa anatunza mtoto wao mmoja ambaye anasema sasa amenona.
“Hatimaye naweza sema nimetulia. Nina yaya wawili wazuri na mmoja ni wa Milla. Sahizi by the way mnaweza notice Milah amenona. Na hata sahizi huwezi muinua hivi vile tulikuwa tunamuinua ovyo ovyo,” Chebby aliongeza.
Aliendelea na kusema binti yake ni mzima na yeye ni mmoja wa watoto wenye afya njema.
Milly Chebby na mume wake Terence Creative wana binti mmoja kwa jina Milla.
Terence Creative na Milly Chebby walifanya harusi ya kitamaduni mnamo 2023.