Aliyekuwa mchekeshaji wa kipindi cha Churchill Show, Mammito Eunice, ameendelea kutoa maelezo zaidi kuhusu ujauzito wa mtoto wa kwanza aliotangaza mapema wiki hii.
Katika chapisho siku ya Jumatano, mrembo huyo mcheshi alidokeza kwamba alipata ujauzito ambao anabeba wakati wa maandamano ya vijana yaliyofanyika nchini Kenya miezi michache iliyopita.
Mammito alibainisha kuwa huenda hakuweza kuficha furaha yake baada ya vijana kuvamia bunge mwezi wa Juni, na hilo likapelekea mimba ambayo anaibeba kwa sasa.
"Maandamano Baby… Baada ya kuingia bungeni, nadhani nilisherehekea sana!!!," Mammito alisema chini ya video aliyochapisha Instagram ikionyesha ujauzito wake.
Mchekeshaji
huyo alifichua hayo alipokuwa akitangaza shoo yake ya ucheshi iliyoratibiwa
kufanyika Desemba 20, 2024.
Katika
tangazo lake, alieleza kwamba anahitaji pesa za kumlea mtoto wake ambaye
hajazaliwa.
"Pata tikiti zako kwa sababu bish anahitaji pesa za nepi," alisema.
Mammito alitangaza habari za ujauzito wake siku ya Jumanne
katika video ya kibunifu ambayo aliichapisha kwenye mitandao ya kijamii.