logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Muthee Ndegenye aibua wasiwasi mitandaoni kwa ujumbe wa kujitabiria kifo

Katika hali ya kutabiri, Ndegenye alidai kuwa kifo chake kitakuwa cha ajabu cha kuhusisha magari mawili ya kifahari aina ya V8 akisema “nitakufa kwa sababu nilifunika dhambi”.

image
na MOSES SAGWE

Burudani02 November 2024 - 13:21

Muhtasari


  • Katika aya nyingine, Ndegenye alifichua kwamba atatoa wimbo wa kuelezea kwa kina chanzo cha kifo chake ambacho alisisitiza kwamba kitatokea hivi karibuni.

Mchekeshaji Mc Muthee Ndegenye amewaacha mashabiki wake wengi katika hali ya utata baqada ya kuandika ujumbe wenye ukakasi kupitia ukurasa wake wa Facebook.

Ndegenye alichapisha picha akiwa ameketi amevaa suti ya samawati akionekana kuwa mwenye mawazo mengi.

Aliambatanisha picha hiyo na ujumbe akitabiri kifo chake ambacho alidai kitatokea siku si nyingi zijazo kupitia ajali ya magari mawili ya kifahari.

Katika hali ya kutabiri, Ndegenye alidai kuwa kifo chake kitakuwa cha ajabu cha kuhusisha magari mawili ya kifahari aina ya V8 akisema “nitakufa kwa sababu nilifunika dhambi”.

“Kabla ya mjaze RIP huku........😢😢 Soon and very soon,I might die...na kifo changu kitakuwa cha kutisha...kitahusisha 2 v8s ..moja itaniblock mbele nyingine upande so sina njia ya kutoroka......nitakufa because nlifunika dhambi. .....hakuna ambaye angetamani kama hayo yatokee..ila nina ndoto mbaya siku hizi...nakuwa mlevi.....samahani.....nimekuandaa tu..sijui tarehe lakini itakuwa hivi karibuni,’ aliandika.

Katika aya nyingine, Ndegenye alifichua kwamba atatoa wimbo wa kuelezea kwa kina chanzo cha kifo chake ambacho alisisitiza kwamba kitatokea hivi karibuni.

“Pia najihurumia...Nlifunika makosa...kesho natoa wimbo wa saa tisa...........wimbo huo utakuwa chanzo cha kifo changu😢😢🙏 Soon...i dont know wen but very soon......Ndegenye will be past tense,” aliongeza.

Jumbe hizi zimewaacha wengi katika hali ya wasiwasi, baadhi wakifichua kwenye upande wa kutoa maoni katika chapisho hilo kwamba Ndegenye hachukui simu zao walipojaribu kumfikia ili kujua nini kinaendelea katika maisha yake.

“Hili ni suala la kina kuliko sisi sote tunavyofikiria.” Martha Mwihaki Hinga aliandika.

“Moyo wangu unaenda kwako rafiki yangu Mc Muthee Ndegenye, bado una mengi ya kukamilisha, wewe ni kijana na mwenye nguvu sana.” Shiro Ann alisema.

“Katika ulimi kuna nguvu ya kifo na uzima. Hili linaweza kutokea si kwa sababu ya nani anayemtisha, bali kwa sababu amekubali. Unahitaji kuibatilisha mwenyewe kwa njia zote, ili hakuna madhara yatakayokupata,’ Lizzbett Gauchuh alimshauri.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved