logo

NOW ON AIR

Listen in Live

“Kulala na wanawake 400 na kurekodi hakukufanyi kuwa lejendari” – Robert Burale

“Tuache uwongo kwa Vijana wetu..Kulala na wanawake 400 na kurekodi sio ubabe, alama ya kweli ya mwanamumke ni jinsi alivyo karibu na kusudi lake,” Burale alisema.

image
na MOSES SAGWEjournalist

Burudani05 November 2024 - 10:51

Muhtasari


  • “Tuache uwongo kwa Vijana wetu..Kulala na wanawake 400 na kurekodi sio ubabe, alama ya kweli ya mwanamumke ni jinsi alivyo karibu na kusudi lake,” Burale alisema.
  • “Na aibu kwa wanawake wanaomsifu bado unakimbilia kwa mchungaji wako kulia mumeo akichelewa kurudi nyumbani,” aliongeza.



Mchungaji Robert Burale amekuwa mtu wa hivi punde kutoa maoni yake kuhusu gumzo linaloendelea kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mwanamume anayedaiwa kurekodi video za wanawake zaidi ya 400 aliolala nao.

Mwanamume huyo kutoka nchini Equitorial Guinea amekuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii tangu wiki hii ilipoanza, uvumi ukiwa kwamba alirekodi video chafu za wanawake zaidi ya 400 alioshiriki nao mapenzi.

Inadaiwa kwamba jamaa huyo alishiriki mapenzi na wanawake wengi wao wakihusishwa kuwa na ukoo kutoka kwa familia ya viongozi wakuu serikalini humo.

Baada ya uvumi huo kuvujishwa mitandaoni, Burale amejiunga na Wakenya ambao wametoa maoni yao kuhusu ripoti hizo ambazo hata hivyo hajizathibitishwa iwapo ni za kweli.

Kwa mujibu wa Burale, wengi wanaomsifia jamaa huy eti ni gwiji wa mapenzi kwa kufanya mapenzi na wanawake zaidi ya 400 wanawadanganya vijana.

Burale ni wa mtazamo kwamba kufanya mapenzi na idadi kubwa ya wanawake na kisha kurekodi wote hakuwezi hata siku moja kumfanya mtu kuwa gwiji.

“Tuache uwongo kwa Vijana wetu..Kulala na wanawake 400 na kurekodi sio ubabe, alama ya kweli ya mwanamumke ni jinsi alivyo karibu na kusudi lake,” Burale alisema.

Mchungaji huyo pia aliwasuta na kuwakashifu vikali baadhi ya wanawake mitandaoni ambao wameonekana kumsifia jamaa huyo kwa kushiriki mapenzi na wanawake wenzao zaidi ya 400.

Burale anasema kwamba si jambo la busara mwanamke kumsifia mwanamume huyo kwa kushiriki mapenzi na wanawake zaidi ya 400 na wakati mume wao anapochepuka kimapenzi, wanakimbi kwenda kwa mchungaji wao kwa ushauri nasaha.

“Na aibu kwa wanawake wanaomsifu bado unakimbilia kwa mchungaji wako kulia mumeo akichelewa kurudi nyumbani,” aliongeza.

Jamaa huyo mpaka sasa hajazungumza chochote japo kuna uvumi kwamba serikali nchini Equitorial Guinea imetoa agizo la kufutwa kazi kwa mfanyikazi yeyote wa serikali atakayepatikana na kashifa ya aina hiyo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved