logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Eric Omondi: Kwa nini niliahirisha kupata mtoto hadi miaka zaidi ya 40

“Baba yangu alikuwa na wake 5 na tuna binamu wengi sana, nafikiri sababu ambayo sikuwa na mbio kuwa na mtoto ni kwa sababu ya maisha niliyokulia na chenye niliona.”

image
na MOSES SAGWEjournalist

Burudani12 November 2024 - 16:13

Muhtasari


  • “Baba yangu alikuwa na wake 5 na tuna binamu wengi sana, nafikiri sababu ambayo sikuwa na mbio kuwa na mtoto ni kwa sababu ya maisha niliyokulia na chenye niliona.”



Mchekeshaji aliyegeukia uanaharakati, Eric Omondi amefichua sababu ya kuahirisha kupata mtoto katika ndoa yake hadi alipofikisha umri wa miaka zaidi ya 40.


Akizungumza kwenye podikasti ya Hey Girl yake Mungai Eve na Liz Jackson, Omondi alisema kwamba alifanya hivyo kimakusudi kutokana na hali ngumu ya maisha aliyoona katika familia yake.


Eric alisema kwamba alilelewa katika familia ambayo baba alikuwa na wanawake 5 na maisha ya kukidhi hitaji la kila mtoto yalikuwa magumu, hivyo asingependa kumleta mtoto duniani kupitia katika maisha ya mateso kama yale aliyopitia yeye.


“Baba yangu alikuwa na wake 5 na tuna binamu wengi sana, nafikiri sababu ambayo sikuwa na mbio kuwa na mtoto ni kwa sababu ya maisha niliyokulia na chenye niliona.”


“Fahamu zangu ziliniambia tu kabla nizae nitahakikisha kwamba nilichopitia na ndugu zangu mwanangu hakipitii. Hivyo muda wote nilikuwa na woga Fulani tu. Juu kuna wakati mimi mwenyewe nilikuwa najitafutia lakini bado nilikuwa nahangaika, hivyo nikasema sasa na nikileta mtoto duniani itakuwaje,” alifafanua.


Eric Omondi na Lynn walipata mtoto wao mwaka jana baada ya kuwa kwenye mahusiano kwa muda.


Penzi lao limekuwa likinyoshewa vidole kutokana na utofauti mkubwa uliopo baina yao kiumri, ikizingatiwa kwamba Lynn ndio mwanzo ako katika miaka yake ya 20s na Omondi ndio amevuka miaka 40.


 


 



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved