Msanii wa gengetone na Mugithi, Peter Miracle Baby
ametoa jibu saa chache baada ya kuonekana kwenye klabu ya starehe akitumbuiza.
Msanii huyo alikuwa mjadala katika mitandao ya
kijamii baada ya kuonekana akiwa kwenye klabu, miezi kadhaa baada ya kuweka
wazi kwamba alikuwa ameanza safari yake ya uokovu.
Akijitetea kurudi katika maisha ya zamani licha ya
kudai kuokoka, Miracle Baby alinukuu Biblia akisema kwamba watu hawafai kumweka
kwenye mizani kutaka kujua kwa nini alionekana klabuni.
Msanii huyo alisema kuwa vipaji vyote vinatoka kwa
Mungu bila kubagua cha injili au cha tumbuizo la dunia, akisema kwamba anataka
kutumia kipaji alichopewa na Mungu kwa njia sahihi ili asije kukosa majibu
machoni pa Mungu siku ya Kiama.
“Nimeona
watu wengi wakihoji kuhusu mimi. Nilirudi kwenye muziki wa kidunia ndio
nimerudi na nataka nizungumzie hicho kipaji kimetolewa na Mungu na ipo siku
ataniuliza nilikupa kipaji ulichofanya nacho ni kipi?”
Miracle Baby alisema.
Kijana huyo alisema kwamba hahitaji kuambiwa chochote
cha kufanya na kipaji chake, akisisitiza kwamba ataendelea kumsifu na kumtukuza
Mungu kwa njia yake aijuayo mwenyewe.
“I'll
still serve the Lord in my own way ..kitu ingine niko na familia inanitegemea I
need to work so that niweze kuwapea basic needs e.t.c so stop judging me coz
wewe mwenye unani judge, uko na makosa kama hujui ndio hii,”
alifoka huku akinukuu Biblia.
“Mathayo 7 : "Msihukumu, msije ninyi
mtahukumiwa; kwa maana jinsi mnavyowahukumu wengine, ndivyo mtakavyohukumiwa;
na kwa kipimo kile mpimacho, ndicho mtakachopimiwa. ukitazama kibanzi kwenye
jicho la ndugu yako, na boriti iliyo katika jicho lako mwenyewe huiangalii?”
alinukuu.
Msanii huyo alikuwa mgeni wa hospitali kwa miezi
kadhaa tangu Januari mwaka huu ambapo alifanyiowa upasuaji mara kadhaa, kama
alivyoeleza mpenzi wake Carol Katrue.
Baada ya kusaidiwa kutoka hospitalini, Miracle Baby
alitangaza kwamba Mungu amemtoa mbali na kwamba ataanza kumtumikia kueneza
injili yake.
Miracle Baby kwa wakati mmoja hata alisema kwamba
angeanza kutumikia Mungu kwa nyimbo za injili kabla ya kujenga kanisa na kuanza
kuhubiri kama mchungaji mkuu.