Mchekeshaji na muigizaji Dj Shiti ameibuka na utani
kuhusu kitu ambacho kimekuwa kikimnyima
usingizi tangu wiki hii ilipoanza.
Kupitia Instagram, Shiti alikiri kwamba amekuwa
akifikiria siku nzima hadi kupata msongo wa mawazo akijaribu kufikiria kuhusu
pazia atakazotumia msanii Khaligraph Jones katika jumba lake kubwa.
Shiti alisema kwamba kila wakati anapojaribu kuketi
chini na kutulia, anajipata akitafakari kiwango cha pazia ambazo rapa huyo wa ‘Mazishi’
atakuwa akishonewa ili kutoshea katika madirisha ya jumba lake la kipekee.
“Na
imagine khaligraph atashonesha Curtains kiasi ganiii 🤔🤔 hiyo
kitu imeni Stress the whole day,” Shiti aliandika katika picha yake
akiwa ameshika kidevu akiwa amekalia kiti kidogo.
Msanii Khaligraph
Jones amekuwa gumzo la mitandao ya kijamii kwa takribani siku 3 sasa baada ya
kuonyesha picha na video za jumba lake kubwa ambalo limezua mjadala mitandaoni.
Baadhi ya watumizi wa
mitandao ya kijamii wamekuwa wakitania jumba hilo wakilifananisha na jumba la
biashara za jumla, huku wengine wakilifananisha na jumba la masomo ya chuo
kikuu.
Hata hivyo, Jones
alijitokeza akisema kwamba maoni ya watu kuhusu jumba lake hayamnyimi usingizi
hata kidogo, akiweka wazi kwamba shida kama hizo ndizo alikuwa akiomba zimfuate
kwa muda mwingi.
"Unaamka unapata unatrend sababu umejenga nyumba kubwa
inakaa kama maduka, Mungu anajua haya ndio matatizo niliyokuwa natamani,"
Khaligraph alisema.
Awali, alidokeza kwamba muundo wa jumba lake huenda
umechochewa na maisha ya kisanii ya rapa wa Marekani, Rick Ross ambaye pia
anamiliki jumba la kipekee nchini Marekani.
Jones alisema kwamba kwa wale ambao hawajafika kwake, wajue
kwamba madhari yenyewe ni kama mtu kuingia Marekani kwa jumba la Rick Ross.
Alionekana kutupa kijembe kwa wakosoaji wa jumba lake akisema
watu wengi hawajazoea majumba ya muundo huo na ndio wanaobwabwaja kwenye
mitandao ya kijamii.
“Hamjazoea hizi settings, hapa ukikuja ni
kama umeingia Amerika, kwa Rick Ross. Heshima ni lazima kwa OG,” Khaligraph
Jones alisema huku akicheka.
Siku ya Jumatatu, Jones alishangazwa na
watu ambao walikuwa wanachapisha picha na video za jumba lake mitandaoni
wakiambatanisha na kauli za dharau kuhusu mjengo huo.