Mchungaji Robert Burale amefichua kwamba aliwahi
nyimwa nafasi ya kuhubiria vijana katika mkutano Fulani wa injili kutokana na
misimamo yake mikali dhidi ya jumuiya ya mapenzi ya jinsia moja, LGBTQ.
Akizungumza na Dr Ofweneke kwenye podikasti ya Lessons
@30, Burale alisema kwamba misimamo yake mikali dhidi ya LGBTQ ilimkosesha
fursa ya kuhubiri baada ya viongozi wa mkutano huo wa injili kumtaka
asizungumzie masuala ya LGBTQ katika mahubiri yake.
Hata hivyo, Burale alisema kwamba alikataa
kusikilisha maelekezo yao na kufunga Biblia yake na kuondoka bila kuhubiria
vijana kwenye mkutano huo.
“Aina
yangu ya injili haikubiliwi katika baadhi ya mimbari. Nimewahi kataliwa
nisihubiri kwa sababu nimetalikiwa, na pia nimewahi ambiwa kwamba ‘tunajua
unazungumza sana dhidi ya LGBTQ, tafadhali kwenye mimbari hii legeza Kamba,
hatuzungumzii masuala hayo hapa’. Niliwaambia mnajua nini, Mungu awabariki. Nikafunga
Biblia yangu na kuondoka,” Burale alisimulia.
Hata hivyo, mchungaji huyo alifafanua kwa kiduchu
kwamba tukio hilo halikumtokea nchini Kenya lakini ni katika nchi nyingine
ambayo aliahidi siku moja atakuja kuiweka wazi na kuzungumzia hali nzima jinsi
ilivyotokea.
Burale alisema kwamba msukumo wake kuhubiri dhidi ya
LGBTQ ni kutokana na idadi kubwa ya vijana Nairobi anaowajua wanatembea na nepi
kwa kulawitiwa.
“Kuna
baadhi ya wanaume kutoka taifa fulani la Afrika Mashariki na jamii Fulani hapa.
Wanachukua wavulana wadogo na kuwalipa Ksh1,000 kwa shoti na wanawaharibu. Vijana
sasa wanatembea na nepi. Vijana wengi sasa hivi wanatembea wakiwa wamejifunga
nepi na mtu Fulani anakuja kusema eti tusikemee suala hilo. Unajua utasema
tusikemee hadi pale litakapofika mlangoni pako,”
Burale alisema.
Awali, Burale alisema kwamba amewahi nyanyapaliwa
mitandaoni kuwa ni iluminati kutokana na mapenzi yake kwa mavazi meusi.
“Wenye
chuki hawawezi kusema chochote cha hakika, kuna mtu aliniita pasta wa iluminati
eti ndio maana nahubiri nikiwa nimevaa nguo nyeusi. Ukweli ni kwamba mimi
napenda nguo nyeusi na nitaendelea kuvaa nguo nyeusi. Mimi navaa suti nyeusi na
hata boxer nyeusi, ni vile tu siwezi onyesha,” Burale alisema.
Burale alisema kwamba matukio kama hayo
yamemfanya kubana idadi ya marafiki zake, akisema kuwa yeye ana marafiki 4 tu.