Mchekeshaji Kendrick Mulamwah ameonyesha maendeleo ya
ujenzi wa jumba lake la kifahari kijijini.
Mulamwah alifurahi akifichua kwamba ujenzi hupo
unakaribia kukamilika, huku akisimulia jinsi ni gharama ghali kumalizia ujenzi
kuliko kuanza.
Mchekeshaji huyo alitania akisema kwamba jumba lake
sasa limefika hatua ya kuzungumza Kizungu, akimaanisha kwamba limenaza kuleta
muonekano wake halisi kama ilivyokuwa kwenye mchoro.
“Maskani inakuja pole pole tu, kumaliza ndio
joto lakini almost done , nyumba inaongea kizugu sasa
. pace ni pole pole tu let no one
pressure you.move slow move correctly,” Mulamwah alisema.
Mtangazaji
huyo wa redio pia alichukua nafasi hiyo kumhongera rapa Khaligraph Jones kwa
ujenzi wa jumba la kipekee viungani mwa mji wa Ngong.
Kwa mujibu wa
Mulamwah, ambacho amekifanya Khaligraph Jones si cha kuchukuliwa kwa mzaha
kwani kujenga jumba mpaka kulikamilisha si kazi rahisi.
“Proud of Khaligraph Jones, kitu umefanya ain’t
easy to achieve. to anyone else out there its all possible - baraka tele ,
Mungu mbele,”
aliongeza Mulamwah.
Mulamwah
amekuwa akishughulika juu chini kukamilisha ujenzi wa jumba lake la kifahari
kijijini Kitale kwa zaidi ya miaka miwili sasa.
Mchekeshaji
huyo alianza ujenzi wa jumba hilo mapema 2022 baada ya kuachana na aliyekuwa
mpenzi wake Carrol Sonie.
Hata hivyo,
kwake amekuwa akipata faraja kwa methali ya pole pole ndio mwendo, akiendeleza
ujenzi wake.
Kwa upande
mwingine, Khaligraph Jones amekuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii kwa wiki
sasa baada ya kuonyesha mjengo wake uliokamilika.
Muundo na
muonekano waq mjengo huo ulizua gumzo mitandaoni, baadhi wakiutania kuwa ni
mkubwa kupita kiasi na kwamba halifahi kuwa jumba la makazi ya kibinafsi bali
jumba la biashara ama taasisi ya masomo.
Khaligraph
alionekana kutoyumbishwa na kauli hizo za husda, akisema kwamba ndoto yake ni
kuishi maisha kama rapa wa Marekani, Rick Ross.
Jones alisema
kuwa anapoona watu wanamzungumzia katika mitandao ya kijamii kisa jumba lake
kubwa, shida kama hizo ndizo alikuwa akiota kumtokea miaka mingi iliyopita.