Msanii na rapa Stevo Simple Boy amegeuza ukurasa wake
wa Instagram kuwa kanisa ya kipekee na kuwapakulia neno mashabiki na wafuasi
wake.
Msanii huyo ambaye aliibuka akiwa amevalia suti ya
samawati na mkononi amejihami na Biblia, aliwahubiria mashabiki wake akisema
kwamba angefurahi kila mmoja wao angemsikiliza na kupata wokovu.
Msanii huyo wa ‘Mihadarati’ aliwataka vijana kutafuta
wokovu ili kujinafasi katika safari ya mbinguni, akiwataka pia kutoingia kwenye
majaribu ya uzinzi haswa wakati huu wa kijibaridi kikali.
“Bwana Yesu asifiwe, watuwangu wa kanisa, mimi kama
Askofu Stevo Simple Boy, nawaambia mpende Mungu sana, muache usherati, muache
mihadarati, muache uzinzi na matendo maovu na mtabarikiwa, au sio,” Stevo
alihubiri huku akimalizia, “okoka tuende mbinguni.”
Msanii huyo amekuwa akitajwa kama mtu mwenye uwezi wa
kufanya mambo ainati kutoka kwa kuimba, ucheshi na sasa hata kuhubiri.
Stevo Simple Boy anatarajia kusherehekea miaka 5 ya
usanii wake, hafla ambayo itafanyika mapema mwezi ujao katika mgahawa mmoja
mjini Kisii.
Msanii huyo aliingia kwa kishindo cha kipekee kwenye
tasnia ya muziki mwaka 2019 ambapo kibao chake cha kwanza ‘Mihadarati’
kilipokelewa kwa shangwe na mbwembwe kutoka kwa mashabiki wake.
Tangu wakati huo, wengi wameshindwa kujizuia kwa
ngoma zake ambazo zinakuwa na ujumbe wa kuchekesha haswa kwa chaguzi za maneno
anayotumia yenye maana fiche.