MBUNGE wa Mumias Mashariki, Peter Salasya amewajibu
wale ambao hawajawahi kutana naye ana kwa ana na ambao wana taswira tofauti ya
muonekano wake vichwani mwao.
Kupitia kurasa zake kwenye mitandao ya kijamii,
Salasya aliweka wazi kwamba kuna baadhi ya watu ambao hawajawahi kutana naye
wanafikiria kwamba yeye ni mtu mweusi na pengine mnene.
Alikanusha madai hayo akisema kwamba yeye ni mweupe
kwa ngozi na pia ni mwembamba lakini wakati mwingine kamera humtoa kuonekana
mweusi hivyo kuwachanganya watu kuusu muonekano wake halisi.
“Kumbe
watu hufikiria mimi ni mu dark skin hehe ni camera tu hunitoa mbaya but am slim
and light skin,” Salasya alisema.
Mbunge huyo alikuwa akiwaelezea watu waliokutana naye
ghafla baada ya kutua jijini Mombasa kwa ajili ya michezo ya wabunge wa Jumuiya
ya Afrika Mombasa iliyoanza Jumamosi.
Watu hao walionyesha furaha na kukutana na Salasya na
kueleza jinsi ambavyo wamekuwa wakifikiria muonekano wake.
Mmoja alisema kwamba yeye amekuwa akifikiria Salasya
ni mtu mweusi mnene kiasi kumbe ni tofauti na yule aliyemuona.
Mbunge huyo wa DAP-K kwa sasa yuko katika vita vikali
na baadhi ya wandani wa chama cha ODM ambapo aliweka wazi lengo lake ni kuhakikisha
amemng’oa kiongozi Raila Odinga katika ukanda wa Magharibi kwa kufifisha
ushawishi wake.
Salasya alimshtumu Odinga kwa kusaliti Gen Z
alipoungana na Ruto wakati Maandamano ya vijana hao yalikuwa yamefika kilele
chake kati ya mwezi Juni na Agosti mwaka huu.
“Tumeshaanza
kufanya zoezi la kutoa elimu ya kiraia, tukiwaambia watu wetu kutoka Magharibi
mwa Kenya Raila Odinga ni nani,” Salasya alifichua.
Mbunge huyo kijana alidai kwamba Odinga
tayari ameitisha kikao na wanachama wa Odinga katika kile alisema ni kuanza
kuwatishia dhidi ya kutonena kwa sauti moja ya muongozo wa chama.
“Na
baada ya kusikia hivyo naambiwa ameita mkutano na wananchama akiwatishia kwa
kutumia kamati za bunge. Ningependa kuwaambia watu kutoka Magharibi, wale
waheshimiwa wanaoenda kumuona, ni kwamba tu kama hawawezi onyesha mshikamano
watatolewa kwenye kamati za bunge,” Salasya
alidai.