NGULI wa muziki kutoka lebo ya muziki ya Next Level
Music, Raymond Mwakyusa maarufu kama Rayvanny ameonesha fadhila zake kwa
mashabiki wake kutoka Kenya kwa kuendelea kumpa sapoti kubwa.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, alichapisha ujumbe
wa kuwashukuru mashabiki wake kutoka Kenya baada ya kujitokeza kwa wingi katika
shoo ya Furaha Fest alikokuwa miongoni mwa wasanii waliotumbuiza.
Akitoa shukrani zake, Rayvanny alifichua kwamba siku
mashabiki wa Kenya watagoma kusapoti muziki wake, basi biashara yake katika
muziki itakuwa imefika mwisho na hatokuwa na budi ila kutafuta kitu kingine cha
kufanya mbali na muziki.
“Mimi
ni Mtanzania 🇹🇿
Napenda mashabiki Wote wanao support Rayvanny Duniani kote, ila siku wakenya 🇰🇪🇰🇪
🇰🇪🇰🇪🇰🇪🇰🇪
wakiacha kusaidia rayikimani yako ni kusaidia rayikimani yako mengi,”
Rayvanny alisema.
Chapisho lake lilijiri siku moja baada ya vurumai
kushuhudiwa katika ukumbi wa Polo ambapo Furaha Fest ilikuwa inafanyika.
Zogo hilo lilijiri baina ya Willy Paul na uongozi wa
Diamond Platnumz ambaye aliishia kuondoka kwa ghadhabu bila kutumbuiza licha ya
kuratibiwa kuwa miongoni mwa watumbuizaji.
Willy Paul alionekana kuendeleza chuki hiyo hadi kwa
Rayvanny, ambapo alikataa kutumbuiza kolabo yao ya pamoja ya ‘Mmmh’ iliyotoka
miaka 5 iliyopita.
DJ alipomchezea Willy Paul wimbo huo wakati
anatumbuiza jukwaani, msanii huyo alimfokea na kumtaka kuweka wimbo mwingine,
huku akiutaja wimbo huo kama ‘takataka’.
Lakini Rayvanny kwa upande wake alisema kwamba japo
Pozee alionyesha dharau kolabo yao, yeye bado anamkubali kama kakake.