MCHEKESHAJI Mammito Eunice kwa mara ya kwanza
amenyoosha maelezo kuhusu ukungu unaozingira mhusika wa ujauzito wake.
Akizungumza na Betty Kyalo kwenye runinga ya TV47,
Mammito alisema kwamba mimba yake ina mhusika mahsusi kwani hakuinunua.
Mchekeshaji huyo alisisitiza hata hivyo kwamba baba
mwanawe mtarajiwa ni mtu na yuko jijini Nairobi lakini akasema hayuko tayari
kufichua utambulisho wake.
“Hii
mimba yangu sijanunua, ni ya mtu tu; ni kijana tu wa watu na ni mtoto wa mtu Fulani,”
Mammito alieleza.
Kuhusu ni kwa nini hayuko tayari kumtambulisha
mhusika huyo kwa mashabiki wake mtandaoni, Mammito alisema kuwa anafanya hivyo
ili kumkinga yeye na pia mwanawe kutoka kwa hukumu hasi za watu wa mitandaoni.
‘Lazima
wafichwe hii Nairobi. Huwezi jua. Useme ndio huyu waseme ooh hakai vizuri na
wengine wamchukue na mimi sasa hivi nina umri wa miaka 31, sitaki kuanza
kuuliza mtu eti rangi uipendayo ni gani, katika huu umri nimeshakua sasa,
unaelewa,” Mammito alifafanua.
Akizungumzia kuhusu uvumi wa kuhusisha mimba yake na
mchekeshaji mwenza, Butita Eddy, Mammito alikanusha kwa haraka akisema kwamba
yeye na Butita ni mambo ya zamani ambayo ytalifika mwisho takribani miaka 4
iliyopita.
Alisema kwamba kabla ya kuamua kubeba ujauzito,
alikuwa anataka mtu ambaye si maarufu mitandaoni na ndiye aliyepata.
“Mimi
na Butita ni maneno ya kale, ni muda mrefu uliopita kama miaka 4 iliyopita. Kwa
huyu, ni mtu ambaye si maarufu mitandaoni. Na nafikiri mtu wa aina hiyo ndiye
nilikuwa nataka, mwenye anajishughulisha na mambo tofauti kabisa na tasnia yetu
ya mitandaoni.”
“Kwa
sababu awali nimeshawahi kuchumbiana na mtu kwenye tasnia hii na nilichagua
kutochumbiana na mtu kutoka hapo tena. Nilichomeka lakini nilijiambia kwamba
ningetaka kitu tofauti. Mtu ambaye ananiambia kuhusu kazi yake yenye sielewi,”
alisema.
Akizungumzia kuhusu shoo yake inayotarajiwa siku 10
zijazo yenye mada ‘Maandamano Baby’ na ni kwa nini aliipa shoo hiyo jina hilo,
Mammito alisema;
“Wakati
niligundua kwamba nina mimba nilifurahia na nikajiambia kwamba ni sharti
niwataarifu mashabiki wangu kuhusu safari yangu ya ujauzito. Mashabiki wangu
wameniona tangu nilipoanza ucheshi nikiwa kama miaka 18 na wameniona nikikua…”
“…na
pia nimekuwa nikizungumza kuhusu kuvunjwa moyo na jinsi wanaume wa Nairobi
walivyo, lakini sasa nina kitu kipya cha kuzungumza, hivyo nikaona niwataarifu
kwa sababu hiki ndicho kitu kikubwa kilichotokea kwangu mwaka huu, sawa na Maandamano
yalivyokuwa tukio kubwa, hivyo nikaona kuuunganisha vitu hivyo viwili litakuwa
jambo zuri.”