MSANII kutoka lebo ya
Konde Music Worldwide, Harmonize amekuwa wa hivi punde kuweka kwenye mizani
suala la kufarakana kwa Willy Paul na Diamond kwenye steji wikendi iliyopita.
Harmonize, ambaye
amekuwa akifuatilia zogo hilo kwa ukaribu japo kimya kimya, alisema kwamba
kilichomkuta Diamond kikimtokea katika shoo yake nchini Uganda, kesi itaishia
polisi.
Msanii huyo alitamba
kwamba akitokea msanii yeyote wa kujaribu kuvuruga shoo yake inayotarajiwa
kufanyika nchini Uganda mwishoni mwa mwaka, basi yeye hatokaa kutulia bali
atamkabili msanii huyo kwa makofi na vibao, kisha shoo iendelee na baadae kesi
isuluhishwe polisi.
Harmonize alisema hakuna
msanii yeyote nchini Uganda atakayejaribu kuvuruga shoo yake au kuisitisha
isipokuwa tu rais wa taifa hilo, Yoweri Museveni.
“Uganda 🇺🇬
team no excuses coming 🏃
kama kuna msani wenu mkorofi mkorofi mwambie ni kabisa atapigwa !!! Nakamata natia vibao!!!
Show itafanyika kisha tutakutana polisi 😏 hakuna wakunizuia kuimba labda
mwenyewe rais @kagutamuseveni mtu mwema sana ❤️ tukutane hapo bange,”
Harmonize aliandika.
Kauli yake ilionekana
kurejelea kilichotokea katika ukumbi wa Polo Club wakati wa Furaha Fest na
kusababisha Diamond kuondoka bila kutumbuiza.
Uvumi wa awali ulidai
kwamba Diamond na Willy Paul walivurugana kila mmoja akipambania muda wa
kuingia kwenye steji.
Hata hivyo, Diamond
katika taarifa yake kwa njia ya video alikanusha uvumi huo akisema kwamba yeye
hangeweza kupigania kuingia stejini kwani tayari alikuwa ameshalipwa.
Msanii huyo alisema kuwa
kilichosababisha yeye kutotumbuiza ni vurugu zilizokuwa zikiendelea kwenye
ukumbi, akisema kuwa muda wote alisalia katika gari lake hadi meneja wake alipoamua
kumrudisha hotelini.
Diamond alisema hakuna
chochote alikipoteza kiasi cha kumtaka kupambania kuingia stejini, akisema
tayari alikuwa amelipwa zaidi ya shilingi milioni 19.
Aliwalaumu waandaaji wa
kuponza shoo kwani walishindwa kutuliza vurugu ili apate nafasi ya kuingia
stejini kuwapa mashabiki burudani.
Alimtaja Willy Paul kama
msanii aliyekuwa akijaribu kulivuta jina lake kwa matope ili akitafuta kiki, huku
akisisitiza kwamba hakuna mahali walikutana na msanii uyo au kubishana kwani
muda wote yeye alikuwa ndani ya gari lake.