MSANII wa Kings Music, Alikiba ameonekana
kutofurahishwa na kauli ya msanii kutoka lebo pinzani ya WCB Wasafi, Mbosso
Khan kwamba yeye [Alikiba] amezeeka.
Mbosso na Alikiba walikuwa katika hafla ya kimuziki
ya mwanasiasa mmoja eneo la Rufiji nchini Tanzania ambapo kila mmoja
alitumbuiza kwa wakati wake.
Baada ya shoo, Mbosso alifanya mahojiano na waandishi
wa Habari ambapo alimtaka Alikiba kuweka pembeni bifu na badala yake kumfuata
Diamond Platnumz leboni Wasafi kwa ajili ya kolabo ya kumaliza uhasama.
Kwa mujibu wa Mbosso, Alikiba sasa hivi ameshakua mtu
mzima na katika uzee wake, hafai kuendekeza bifu la kimuziki na Diamond.
Mbosso alisema kwamba yeye alishawahi kutembea katika
lebo ya Kings Music na kukutana na Abdukiba, mdogo wake Alikiba.
Hivyo, alimtaka Alikiba pia kurudisha mkono kwa
kutembea leboni WCB Wasafi na kumkuta Diamond ili wamalize uhasama.
“Alikiba
ni vile hajaongea tu vizuri na mwamba yule [Diamond]. Angekuja kule angefanya
tu kolabo. Anakaribishwa kule. Mimi nishawahi enda Kings Music, anatakiwa aje
yeye sasa,” Mbosso alisema kwa sehemu.
“Eeh
bwana mzee, unazeeka, hayo mambo hayatakiwi sasa hivi, njoo kule [WCB Wasafi]
ufanye kolabo,” aliongeza.
Hata hivyo, Alikiba kwa kauli ya kutoridhishwa na
kuitwa mzee, alisema kwamba yeye hana haja yoyote ya kuenda Wasafi kwani ujio
wa Mbosso Kings Music haukuwa kwa ajili yake.
Alikiba alisema pengine Abdukiba ndiye tu anaweza
kutembea Wasafi lakini si yeye.
“Kwa
nini kwanza mimi niende Wasafi? Kwa sababu yeye alikuja kwa ajili ya Abdukiba
inabidi tu Abdukiba yeye ndiye aende kule. Hakuna sababu ya mimi kunifanya niende
kule not unless nataka kufanya kazi. Lakini sina kazi. Sina maana kwamba
nashindwa kuenda lakini sina kazi ya kufanya,”
Alikiba alijibu.
“Mimi
sina sababu ya kushindana na zamani nilishawahi kutukanishwa hadi na mamangu
matusi ya nguoni, wakaona hilo sijibu na sasa hivi wamekuja na kampeni nyingine
kwamba nimeisha, sijui nimezeeka. Wanaosema nimezeeka, muda utasema na wakae
wakijua kwamba uzee ni kifo,” alimaliza.