
Msaani wa bongo Harmonize ametoa onyo kali kwa wasaani wa Uganda dhidi ya kuvuruga tamasha lake litakalofanyika nchini humo. Hii ni baada ya Diamond kubishana na Willy Paul wakati wa tamasha ya Furaha Fest nchini Kenya.
Harmonize amesems kwamba atahakikisha kuwa tamasha hilo nchini Uganda litakuwa lenye mafanikio bila vurugu ya aina yoyote akisema kuwa hatakubali vurugu kutokea akiahidi kukabiliana na msaani yeyote atakaye jaribu kuzua sintofahamu. Harmonize alidokeza haya akirejelea tokeo lililotokea nchini Kenya hivi majuzi wakati Diamond Platnumz alikosa kutumbuiza mashabiki akikiri ukosefu wa usalama.
Tukio hilo lilifichua malalamiko yanayoendelea kuhusu kutokuwa na usawa katika tasnia ya usanii hasa wasanii wa Kenya na Tanzania, huku Willy Paul akiwatuhumu waandalizi wa tamashi hilo kuwapendelea wasanii wa Tanzania.
Diamond Platnumz alikanusha madai hayo, akihimiza umoja na kufanya kazi kwa bidii badala ya kuchochea migawanyiko. Alisema kuwa tendo la Willy Paul lilisukumwa na kiu ya kutafuta kiki na umarufu.