Mchekeshaji na mtangazaji wa redio, Kendrick Mulamwah
amefichua jumla ya pesa ambazo amekuwa akiwekeza kidogo kidogo kwa kipindi cha
mwaka mmoja.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Mulamwah
alifichulia mashabiki wake kwamba alianza safari ya kutenga shilingi elfu 3
kila siku Desemba 15 mwaka jana na mwaka mmoja baadae amevunja kibubu.
Baada ya kuvunja kibubu chake, Mulamwah alisema
kwamba shilingi elfu 3 yake ya kila siku imezalisha jumla ya milioni 1.1 baada
ya mwaka.
“God
is great - 3k per day savings Challenge imekamilika kwa 2024. 💪🔥
ilianza tarehe 15 Desemba mwaka jana kuweka pole pole tu. Umeweka ngapi? kama
hujaweka tuanze wote for next year,” Mulamwah alisema.
Mulamwah alitumia fursa hiyo kuwashauri mashabiki
wake kuwa na hulka ya kuwekeza hela kidogo kidogo akisema kuwa hiyo ndio njia
pekee ya kujisaidia.
Alisema kwamba hizo hela zake sasa ataongeza shamba.
“Haijalishi
ni kiasi gani ata 20, 50, 100, 1k kwa siku ni sawa. Jaribu kuweka pesa kwa
sababu itakuokoa kila wakati. Wacha tuongeze kaploti sasa,”
Mulamwah alisema.
Hata hivyo, kilichowashangaza wengi ni kauli yake
kwamba amekuwa akiwekeza shilingi elfu 3 kwa kila siku kwa mwaka mzima.
Mmoja alimuuliza ni kazi gani hiyo alipata ya
kumwezesha ku’save 3k kila siku na Mulamwah alijibu akisema kwamba ni kazi za
mtandaoni huku akimtaka kujiunga naye kwa mafunzo jinsi ya kutengeneza hela
kiasi hicho na zaidi kwa siku.
“Uliwezaje
kupata kazi ambayo unaweza kuwekeza 3k kila siku?”
shabiki mmoja alimuuliza.
“Tunavumilia
tu matusi huku online tukijua tunachotaka,”
Mulamwah alijibu.