MKE wa Marioo, Paula Kajala amechukua kwenye mitandao
ya kijamii kulalamika jinsi picha yake ilivyotokea wakati anahudhuria hafla ya
mtangazaji wa Wasafi FM, Juma Lokole.
Lokole alichapisa picha hiyo akiwa na Paula
ikimuonesha mrembo huyo mama wa mtoto mmoja akiwa na muonekano usio wa kawaida
kwa mashabiki wake.
Paula alitokea akiwa amevaa nguo kubwa refu iliyokaa
kama inamvaa na kuficha kabisa umbo lake zuri, jambo lililowafanya mashabiki
wake kuduwaa.
Paula alielekea kwenye picha hiyo katika ukurasa wa
Juma Lokole na kuweka wazi hisia zake za mafadhaiko, akisema ajapenda jinsi
mpiga picha alivyoitoa picha yake.
Kwa mujibu wa Paula Kajala, mpiga picha aliificha, au
kuififisha shepu lake na kumfanya kuonekana kama mama tu aliyepotelea ndani ya
dera.
“Mpiga
picha kapeleka wapi shepu yangu sijapenda😂💔😩,”
Paula Kajala alimaka.
Paula ameolewa mwaka mmoja tu uliopita kwa msanii Marioo na
tayari wana mtoto mmoja.
Katika mahojiano ya hivi majuzi, mrembo huyo wa muigizaji
mkongwe wa filamu za Uswahilini, Fridah Kajala Masanja alisema kwamba angependa
sana kama mpenzi wake angeirasmisha ndoa yao kabisa kwa harusi.
Alipoulizwa ni kipi anachokipa kipaumbele kati ya kurudi
shuleni kumalizia masomo na kufunga ndoa, Binti Kajala alisema bila kuwaza mara
mbili mbili kwamba angechagua ndoa kwanza, masomo baadae.
“Nitaendelea na masomo, nasubiri Amarah akue kwanza. Hiyo inawezekana.
Mimi nataka niendelee kusomea fasheni kwa sababu ndicho kitu ambacho nakipenda.
Ninataka kujiendeleza kwenye hilo,” Paula Kajala alisema.
“Hata hivyo bado mipango ya ndoa naitaka
sana. Nataka kuolewa kwanza masomo baadae,” aliongeza.
Marioo alipoulizwa kuhusu hoja hiyo ya mpenzi wake, alikiri kwamba ni
suala la muda tu kwani sehemu kubwa wameshaifanya tayari ikiwa ni pamoja na
kuonana na kujuana na wakwe, katika shughuli ya kutambulisha jinsia ya mtoto
wao miezi michache kabla ya kuzaliwa kwake.
“Suala na ndoa ni jambo jema, na sisi
tumeshakuwa familia. Katika vitu vilivyotokea hapa, ina maana suala la ndoa ni
suala dogo sana. Ni suala tu la kuamua, na sheria tuwe tushaifuata maana vitu
vingi vya msingi tumeshavifanya kwa hiyo imebakia tu sisi kusema kwamba jamani
tarehe Fulani tunataka tuoane, tufunge pingu za maisha,” Marioo alikariri kauli ya mpenziwe.
“Nitamuoa kwa sababu mwanzo nampenda, pili
amenizalia binti mzuri na naheshimu uamuzi wake. Kwa hivyo, kama hitaji lake ni
ndoa tu hilo ni suala dogo na limeisha,” Marioo aliongeza.