Msanii wa Mugithi, Samidoh ameumwaga moyo wake wa
shukrani kwa mashabiki wake baada ya kuufanya wimbo wake mpya kushikilia
kidedea katika nyimbo maarufu kwenye YouTube.
Samidoh aliachia wimbo wake mpya wa Wendo wa Ihera
takribani wiki moja iliyopita, na licha ya kuimba kwa lugha ya Agikuyu, wimbo
huo umeibuka kuwa pendwa miongoni mwa Wakenya wa matabaka mbalimbali.
Wimbo huo unazungumzia mapenzi ya sumu kutoka kwa
mpenzi mwenye hulka mbaya na ndani ya siku tano tu, tayari umetazamwa zaidi ya
mara milioni moja kwenye jukwaa la YouTube.
Samidoh alichukua kwenye kurasa zake katika mitandao
ya kijamii akishukuru mashabiki kwa kumfikisha hapo, akisema kwamba hiyo ni
rekodi mpya katika kariha yake ya muziki.
Alisema pia kuwa kando na wimbo kutazamwa mara
milioni moja, ulimvutia mashabiki wengi na tayari amefikisha mashabiki
waliojisajili kwa chaneli yake hadi nusu milioni.
“Mashabiki
wapendwa, Huenda nisiweze kamwe kukushukuru ya kutosha kwa jinsi unavyoniunga
mkono, kila wakati mwingine. Wakati huu nikiwa na WENDO WA IHERA~Mapenzi ya
Sumu, nilijihatarisha na kuamua kujaribu kitu nje ya eneo langu la faraja, Kusema
kweli Mapokezi yako yameniacha nikiwa nimeshangaa, kunyenyekea na kunitia moyo.”
“Utazamaji
wa MILIONI 1 kwenye Youtube ndani ya Siku 5!!ni REKODI MPYA kwangu na bonasi ya
mashabiki zaidi ya 500k ili kuiongeza na bado inavuma kwa nambari 1 !!Huyu
anaweza kuwa Mungu pekee!! Mifuko yako Isikauke Kamwe na Mungu akutane na wewe
kila wakati kwenye hitaji lako,” Samidoh aliandika.