MSANII STEVO SIMPLE BOY amefunguka kuhusu mipango yake kuelekea siku ya wapendanao ambayo itaadhimishwa mwezi ujao, Februari 14.
Katika mahojiano na Trudy Kitui, Stevo Simple Boy
alisema kwamba tofauti yake na watu wengi, haamini katika mapenzi ya mwanamume
na mwanamke bila kuoana rasmi.
Akitetea msimamo wake, Stevo alisema kwamba mapenzi
ya bila kuoana yanaweza isha wakati wowote tu shida inapotokea, tofauti na ndoa
ambayo itadumu kwa muda baina ya mawimbi.
“Unajua
tofauti yangu na wengine, kuna boyfriend na girlfriend halafu kuna ndoa. Hivyo vitu
ni tofauti sana, mimi huwa naangalia ndoa kwa sababu unajua girlfriend atakuja ‘ooh
Stevo nakupenda...’ halafu anasepa. Lakini mke anafaa apende mtu wake kwa hali
zote,” Stevo alisema.
Rapa huyo alisema kwamba nyakati za sasa kimapenzi ni
tofauti na zamani, japo alikubaliana na dhana kwamba kabla wapenzi wawe
wanandoa, ni sharti waanze kama girlfriend na boyfriend.
Stevo alisema kwamba vijana wa siku hizi wanaanza
kualikana kwa ‘sleepover’ hata kabla ya kila mmoja kujua nyumbani kwa mpenzi
wake.
“Ukiangalia
mambo ya kitambo na siku hizi ni tofauti. Kama ni msichana anapenda mwanaume
ama mwanamume anapenda msichana, anafaa ampeleke kwao familia imuone na kumjua.
Lakini haya mambo ya Sleepover hapana. Hayako kwa Biblia,”
Stevo alisema.
“Mimi
huwa sileti msichana kwangu kwa sleepover kwa sababu hiyo haiko kwa Biblia. Kwa uelewa wangu, kama ni yule mrembo ambaye
hatujajuana vizuri na anataka kuja kunitembelea, akuje tu mchana anione na
apange nyumba na jioni ikifika aende kwake,”
Stevo aliongeza.
Simple alisisitiza kwamba hawezi mkubalia mrembo kuja
kwake kulala naye akisema kwamba, “shida iko, kwa sababu kuna majaribu. Naweza jikuta
nimefanya mambo ambayo hayafai.”
Alipoulizwa ni lini mara ya miwsho alishiriki
mapenzi, Stevo alijibu kwa utani akisema, “Ni kitambo sana, siwezi sema” na
kusisitisha kwamba yeye kula tunda ni hadi siku ya ndoa.
Msanii huyo alifichua kwamba mwaka jana alipata
mpenzi wakapendana lakini kwa bahati mbaya mambo yakaenda mrama na hivyo
akaamua anatulia hadi pale atakapompata anayemfaa.