TIKTOKER Rachel Otuoma amewashukuru wanajamii ya TikTok kwa kusimama naye katika takribani kipindi cha miaka 5 ya ugonjwa wa marehemu mumewe, mwanasoka Ezekiel Otuoma.
Mrembo huyo alizungumza
kwa ujasiri wakati wa mazishi ya mumewe Jumamosi Janauri 11 katika kaunti ya
Siaya na kuwashukuru TikTokers kwa kusimama naye kuhakikisha Otuoma hakuwahi
kosa dawa wala chakula katika kipindi chote cha ugonjwa wake.
“Ningependa kushukuru
kila mtu, na haswa familia yangu ya TikTok, wueh! Nyinyi watu mmenishikilia
kama Otuoma yuko, mmenishikilia kama sasa hivi vile hayuko… tiktokers, ahsante
za dhati kwenu,” Rachael alishukuru.
“Ningekosa hata dawa,
nilikuwa naenda hapo kwa hiyo TikTok, nitachambwa lakini kuna mmoja
atajiotokeza anunue dawa. Hivyo TikTok ni familia yangu. Sikuwahi kosa hata
chakula, kama niko hapo TikTok. Otuoma alikuwa anwafinyia jicho, anawatabasamia
na mlikuwa mnafurahia, hivyo kwangu TikTok ni familia kubwa sana,”
alisema.
Rachael alisema kwamba
mwaka huu ndio wangetiiza miaka 10 ya ndoa na Ezekiel Otuoma, huku akimtaja
kama mwanamume aliyempa heshima ambayo wanawake wengi hawapati maishani.
“Mkiangalia, hapa si
kwamba ninamzika mume wangu kumsahau, hii ni kama kumbukumbu ya 10 ya ndoa
yetu. Huu mwaka tungeadhimisha miaka 10. Mkiniangalia hivi mimi ni mwanamke
mkakamavu sana. Hakuna kitu kingine kinaweza nitingisha juu ya huyu mwanamume.”
“Nitaendelea kumpenda
huyu mwanamume hata kama ako hapa chini, huyu mwanamume alinipa heshima yenye
wanawake wengine hata hampati hapo nje. Na bado nitampa hiyo heshima hata kama
hayuko nando yangu,” Rachel aliomboleza Ezekiel Otuoma.