logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Chris Brown Aguswa Na Video Ya Vijana DR Kongo Waliohukumiwa Kunyongwa

Video ambazo zimekuwa zikisambaa zinaonesha vijana hao wakiwa katika hali ya majonzi wakati walikuwa wanasafirishwa kwenda kunyongwa.

image
na MOSES SAGWEjournalist

Burudani16 January 2025 - 12:29

Muhtasari


  • Chris Brown alichukua kupitia Instagram yake na kusema kwamba video hiyo inakata maini sana na inaashiria jinsi utu na ubinadamu umeyeyuka miongoni mwa watu.
  • “Nyinyi wote mumeona video zile zinazotoka nchini Congo? Kitendo kile kinavunja moyo sana na kinakosa utu,” Chris Brown alisema.



MSANII wa Marekani, Chris Brown ameguswa na video zinazosambaa kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zikionyesha hali ya kutamasha ya vijana waliohukumiwa kunyonywa.


Awali tuliripoti kwamba zaidi ya vijana 170 wanaoaminika kuwa wanachama wa kundi la Kuluna Gang linalwahangaisha watu mijini walipatikana na hatia na kuukumiwa kifo kwa kunyongwa.


Video ambazo zimekuwa zikisambaa zinaonesha vijana hao wakiwa katika hali ya majonzi wakati walikuwa wanasafirishwa kwenda kunyongwa.


Chris Brown alichukua kupitia Instagram yake na kusema kwamba video hiyo inakata maini sana na inaashiria jinsi utu na ubinadamu umeyeyuka miongoni mwa watu.


“Nyinyi wote mumeona video zile zinazotoka nchini Congo? Kitendo kile kinavunja moyo sana na kinakosa utu,” Chris Brown alisema.


Kwa mujibu wa mashirika ya Habari ya kifamaita, Sabini kati ya wafungwa hao walisafirishwa siku ya Jumapili wiki jana, Waziri wa Sheria wa Kongo Constant Mutamba alisema, akiongeza wafungwa wengine 102 ambao tayari wamepelekwa katika gereza la Angenga katika jimbo la kaskazini la Mongala.

Vijana hao wa kati ya miaka 18-35 wamepatikana na hatia ya wizi wa kutumia silaha na wanajulikana kama "Kulunas" au "majambazi wa mijini."

Wana umri wa kati ya miaka 18 na 35, Mutamba alisema katika taarifa. Hakusema ni lini mauaji yatafanyika


Japo taarifa zingine zinasema vijana hao bado hawajanyongwa, vyanzo vingine vinadai kwamba angalau 100 kati yao wameshauliwa.


Kongo ilifuta hukumu ya kifo mwaka 1981, lakini ilirejeshwa mwaka wa 2006. Unyongaji wa mwisho ulifanyika mwaka wa 2003.

Mnamo Machi 2024, serikali ya Kongo ilitangaza kuanza tena kwa adhabu ya kifo katika kesi za uhaini zilizofanywa na wanajeshi.

Mnamo Mei, wanajeshi wanane walihukumiwa kifo, na mnamo Julai, wanajeshi 25 walitiwa hatiani kwa makosa kama hayo. Hakuna anayejulikana kunyongwa.






 


 



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved