MCHUNGAJI wa kanisa la Neno Evangelism Centre, James Maina Ng’ang’a amewarai wanawake na haswa wale walioko katika ndoa kukoma kutumia mitandao wa Facebook.
Akizungumza katika mahubiri yake siku mbili
zilizopita, mchungaji huyo alidai kwamba mitandao ya kijamii na haswa mitandao wa
Facebook unatumika kama mawindo na shetani.
Mchungaji huyo alisema kwamba watu wengi wanaoabudu
shetani wamejaa katika mitandao wa Facebok wakitafuta watu wa kuajiri katika Imani
yao, lengo kuu likiwa wanawake wa watu.
“Mnajua
jinsi wanaunganisha watu kwenye ‘devil worshipping’? Kuna devil worshipper,
kuna iluminati, kuna wachawi na kuna wazimu. Unajua siku hizi wanafanya nini? Wanakuja
kwa Facebook, na ndio naambia kina mama wale ambao hamna kitu mnafanya tokeni
Facebook,” James Ng’ang’a alisema.
“Hapo
Facebook kuna uchawi ambao hamtaweza. Wake wa watuv tokeni Facebook, hapo kuna
vitu ambavyo hamtaweza. Msifanye mchezo na Facebook, unaenda kote duniani. Na kuna
watu hapo wanafungua link na anakutumia ujumbe, ukifungua huo ujumbe tu,
nyingine huwa zimeandikwa ‘hi’. Ukishajibu tu kuna vitu wanafanya unajikuta
tayari umeshaingia kwao,” alichambua.
Ng’ang’a alieleza kwamba baadhi ya watu hao hutumia
wanawake warembo ambao hujifanya kuwa wanatafuta wanaume wa kuwa marafiki zao.
Hata hivyo, hii si mara ya kwanza kwa hekaya kama
hizo kuenezwa kwamba mitandao ya kijamii inatumika kuwachukua watu katika
itikadi zisizostahili.
Ni dhana ambazo imekuwepo kwa muda japo hatuwezi
kubaini ukweli wake.