WIKENDI iliyopita, maafisa 217 zaidi wa Kenya walisafiri kwenda Haito kujumuika na wenzao katika kuleta utulivu katika mitaa ya mji mkuu wa Port-au-Prince.
Katika video iliyoenezwa
kwenye mitandao ya kijamii baada ya kufika kwao, maafisa hao walionekana
kuwatia moyo wananchi wa taifa hilo la Carrebian kwa nyimbo za kishujaa.
Polisi hao waliimba
wakitangaza ubabe wa Kenya katika kulinda amani wakisema Kenya ni mambo mbaya.
“Sisi hao tumefika,
Kenya mambo mbaya tena sana,” polisi hao waliimba kwa sehemu.
Maafisa hao 217 waliagwa
na waziri wa usalama wa ndani Kipchumba Murkomen kuelekea Haiti kuongeza nguvu
na wenzao zaidi ya 400 walioondoka nchini mwaka jana.
“Niliagana na kikosi cha
pili cha maafisa wa polisi wa Kenya kwenye Misheni ya Kimataifa ya Usaidizi wa
Usalama (MSS) nchini Haiti. Maafisa hao 217 wataimarisha kundi la kwanza la 400
waliotumwa mwaka jana katika taifa hilo la Karibea kurejesha amani,”
Waziri Murkomen alisema kupitia X.
Ujumbe huo unaoongozwa
na Kenya umepata mafanikio makubwa katika kupunguza ghasia za magenge, na
kujipatia sifa kote ulimwenguni, ikiwa ni pamoja na tawala zinazotoka na
zinazokuja za Marekani, waziri huyo alifichua.
“Kujitolea kwetu kwa
dhamira hii ya kihistoria ni thabiti na tutaendelea kuhamasisha usaidizi wote
muhimu wa kimataifa ili kufanikiwa,” Murkomen aliongeza.
Baada ya kutua nchini
Haiti, Wanajeshi wa ziada katika Misheni ya Kimataifa ya Usaidizi wa Usalama
(MSS) walipokelewa na Waziri Mkuu Alix Didier Fils-Aime na maafisa wengine wa
serikali.
Waziri Mkuu alipongeza
uimarishaji huo kama hatua muhimu katika kurejesha utulivu nchini.
Kikosi hicho kiliandamana
na Naibu Mshauri wa Usalama wa Kitaifa Bw. Joseph Boinnet, Naibu Inspekta Mkuu
wa Huduma ya Polisi ya Utawala, Bw. Gilbert Masengeli, na Kamanda Mkuu wa
Kitengo cha Huduma, Bw. Ranson Lolmodooni.