Kulingana na sheria mpya ya shikisho linalosimamia ligii kuu ya mabingwa ulaya UEFA. Mapambano yanahusisha timu 36.
Kila timu itacheza michuano minane. Mechi nne zitapigwa nyumbani na zingine nne zitapigwa ugenini. kulingana na kundi la timu husika.
Baada ya mzunguko huo, timu nane bora zinaingia moja kwa moja kwenye raundi ya 16.
Kisha timu namba 9-24 zitapiga mechi za kutowana nyumbani na ugenini, nane zinazoshinda zinaungana na nane za kwanza katika mchuano wa kumi na sita.
Kufikia sasa baadhi ya vilabu ambavyo tayari vimeshaondolewa kwenye mapambano haya kutokana na alama zao chache ni pamoja na RB Leipzig ya Ujerumani, Slovan kutoka Slovakia, Young Boys ya Usizwi, Blogna ya Italia, Red Star ya Serbia na Sturm Graz ya Australia.
Timu ambayo inaongoza, kwa sasa ni Liverpool ya Uingereza ambayo ina alama 21 na imebakisha mechi moja dhidi ya PSV.
Barcelona wanawafwata kwa karibu wakiwa na alama 18 baada kuwapiga Benfica 5-4 katika mchuano wao wa jana. Wamebakisha mechi moja dhidi ya Atalanta kabla ya kukamilisha msururu wao wa makundi.
Ushindi wa Barcelona katika mechi yao ya mwisho huenda ukawaweka kileleni iwapo Liverpool watapoteza maana ushindani wao ni wa alama mbili tu pekee.
Wanabunduki wanashikilia nafasi ya tano wakiwa na alama 13. timu hio ya wingereza bado imebakisha mechi mbili. Ushindi wa mechi hizo mbili utawapa nafasi ya kumaliza wa tatu katika msururu wa makundi.
Aston Villa ya Uingereza pia imekua katika nafasi nzuri ya kumaliza nane bora lakini kupoteza dhidi ya AS Monaco uliwaacha nambari ya nane, kufaulu kwao kutategemea michuano iliyobaki.
vijana wa Pep Gadiola ambao hawajakua na matokeo mazuri musimu huu wanashikilia nafasi ya 24. Nafasi ambayo ndio ya mwisho kabisa ya kuwapeleka katika michuano ya kutowana ili kufuzu katika mzunguko wa 16.
Manchester City ambao wako na alama nane katika ligii hi ya mabinwa wamebakisha mechi mbili za mwisho.
Usiku wa leo Jumatano 22 watamenyana na Paris Saint Germain ya Ufaransa ianayoshikilia nafasi ya 26 na alama 7. Alama moja tu nyuma ya Man City. Mchuano ambao unatarajiwa kuwa wa mapambano makali kwani Gadiola na Luis wote wanapigania nafasi bora.