MWANAMKE mmoja amewazuzua watumizi wa mitandao ya kijamii baada ya kufichua kile alichokiita habari njema kwake.
Mrembo huyo alichukua furaha yake kwenye mitandao wa
TikTok na kuwafichulia mashabiki wake kwamba hatimaye amepata nafasi katika
chuo kimoja kikuu ya kusomea taaluma ambayo amekuwa akitamani.
Mwanamke huyo alisema kwamba kwa muda mrefu, ilikuwa
ni ndoto yake kusomea fani ya jinsi ya kutunza maiti na sajili nzima ya
mazingira ya makafani.
Alisema kwamba baada ya kutuma maombi, hatimaye chuo
kikuu kimoja kilikubali kumchukua na kumpa mafunzo hayo katika kitivo hicho
ambacho hakiwavutii wanafunzi wengi.
Katika video hiyo, alionyesha uso wake na nukuu
iliyowaacha wengi kushangaa. Aliandika: "Nimekubaliwa katika shule ya
ndoto yangu."
Klipu hiyo ilipocheza, ilionyesha arifa ya
uandikishaji kwenye simu yake, ikithibitisha kozi hiyo isiyo wa kawaida.
Chapisho hili lilipata umaarufu mtandaoni kwa haraka,
na kuibua hisia nyingi kutoka kwa watu waliohusika ambao walikwenda kwenye
sehemu ya maoni ili kushiriki mawazo yao.
INNOCENT ❤️🥶☠️💰: “Mafunzo ya Sayansi ya chumba cha
maiti ni kozi nzuri sana Yo Yo natania 😂. Hakuna idara hii shule yangu
haipati 🤦😂."
ELYON♠️🥷🏿♌:
"kipi kitakuwa sayansi ya kuhifadhi maiti 😂😂."
Nchini Kenya, miaka miwili iliyopita, chuo anuwai cha
mafunzo ya uuguzi, KMTC kilitangaza kuanzishwa kwa kozi ya Wahudumu wa mochari.
“Ulituuliza,
tukakusikiliza! Chuo sasa kitakuwa kikitoa Diploma ya Sayansi ya Maiti kuanzia
Machi 2023. Ni kozi ya kwanza kabisa katika Afrika Mashariki na Kati.”
“Mafunzo
hayo huchukua muda wa miaka 3, huku wale ambao tayari wana cheti katika kozi
moja kutoka taasisi nyingine zinazotambulika watajiunga na kozi ya uboreshaji
ambayo huchukua miaka miwili. Kwa wanafunzi wa shule ya awali, alama ya wastani
ya C- katika KCSE inahitajika huku Cheti cha Sayansi ya Hifadhi ya Maiti ni sharti
kwa wanafunzi walio kazini,” KMTC walitangaza
kupitia ukurasa wao wa Facebook Januari 2023.