MBUNGE wa Likoni Mishi Mboko ameisifia bima mpya ya matibabu ya SHA akisema kwamba ina manufaa zaidi kuliko bima ya zamani ya NHIF.
Akizungumza katika mkutano mmoja kwenye video ambayo
imekuwa ikienezwa kwenye mitandao ya kijamii, mbunge huyo kutoka pwani alisema
kwamba manufaa mapya kwenye SHA yanastahili hongera na heko kwa rais William
Ruto.
Mboko alisema kwamba kutokana na mazuri yanayokuja na
SHA, anataka pia kuzaa mtoto wake wa mwisho na kumpa jina la rais William Ruto.
“Kina
mama tutazaa ama hatuzai? Mimi pia nataka nizae mimba yangu ya mwisho nimtaje
Dkt William Ruto. Ndio, nimtaje maanake SHA iko. Shida iko wapi kama kuna SHA?”
Mboko alihoji.
Aliendelea kudadavua mazuri ambayo mpango huo mpya wa
afya unawapa wananchi akisema kuwa hilo halimpi tatizo katika kutaka kupata
mtoto mwingine tena.
“Kama
nikizaa na kisu (siombi hilo) nalipiwa elfu 30 kwenda mbele, nikizaa kwa njia
ya kawaida, nalipiwa shilingi elfu 10. Kitambo ilikuwa ni Sh2,500 na Sh5,000
kwa upasuaji, kisha bado tunataka kutia porojo na propaganda, jamaa wakati wa
propaganda si sasa jamaa,” Mboko alieleza.
Sheria ya Afya ya Jamii (SHA), iliyotiwa saini na
Rais Ruto kuwa sheria mnamo Oktoba 2024, inalenga kubadilisha Hazina ya Kitaifa
ya Bima ya Afya (NHIF) na kuweka mfumo mpana zaidi.
https://www.instagram.com/buzzroomkenya/reel/DFLYlUCS_xT/
Mpango huo mpya unatanguliza fedha nne ambazo ni:
Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii, Mfuko wa Huduma ya Afya ya Msingi, Mfuko wa
Dharura, Sugu na Ugonjwa Mgumu, na Mfuko wa Wakala wa Afya wa Kidijitali.
SHA imeundwa ili kuhakikisha ufikiaji wa huduma ya
afya kwa wote, haswa kwa watu walio hatarini kama vile wanawake wajawazito,
watoto, na familia zenye kipato cha chini.
Tofauti na NHIF, SHA inashughulikia huduma kama vile:
uchunguzi wa hali za kawaida za afya kama vile saratani, vifaa vya usaidizi kwa
wagonjwa walio na ulemavu wa kudumu, wa kimwili au wa hisia na matibabu ya
dharura ikiwa ni pamoja na bima ya ufufuaji na uimarishaji wa hali mbaya.