GWIJI wa muziki wa Nigeria, Innocent Idibia, maarufu kwa jina la 2Baba, ametangaza kuwa yeye na mkewe Annie Macaulay wametengana na kwa sasa wamewasilisha kesi ya talaka.
2Baba alitumia akaunti yake ya Instagram siku ya
Jumapili kushiriki habari hizo na mashabiki wake.
Aliandika, "Habari kwa watu wangu wazuri wa
mashirikisho yote. Kweli, jambo hili ninalopaswa kusema ni fupi lakini pia
refu…Mimi na Annie Macaulay tumetengana kwa muda sasa, na kwa sasa
tumewasilisha kesi ya talaka.”
"Nitatoa taarifa kwa vyombo vya habari hivi karibuni
ili kusema hadithi yangu. Sio kwa sababu ni haki ya mtu yeyote kujua kuhusu
maisha yangu binafsi lakini kwa sababu ninawapenda watu wangu na ninahitaji
wajue kutokuwa na hatia au kosa langu. Endelea kubarikiwa watu wangu. Nawapenda
nyote.”
Kumbuka ndoa yao imekumbwa na uvumi wa talaka baada ya Annie
kumshtaki 2Baba kwa kutokuwa mwaminifu.
Hata hivyo, baadhi walihisi kwamba taarifa hiyo si ya kweli
na kudai akaunti yake ilidukuliwa.
Katika sasisho, Idibia amekiri binafsi kuchapisha tangazo
hilo kuhusu kutengana kwake na kuachana na mkewe, Annie Idibia.
Katika video iliyoshirikiwa kupitia hadithi yake ya
Instagram siku ya Jumapili, mwimbaji huyo alizungumzia mzozo huo, akisema,
"Ndio, wabariki watu wangu wote. Hakuna mtu aliyedukua akaunti yangu.”
Ufichuzi huu umekuja baada ya mitandao ya kijamii kuzua
tafrani wakati ujumbe wa Instagram kutoka kwa akaunti iliyothibitishwa ya 2Baba
ulitangaza kutengana kwa wanandoa hao.
Chapisho hilo lilisomeka, “Sawa, jambo hili ninalopaswa
kusema ni fupi lakini pia refu. Mimi na Annie Macaulay tumetengana kwa muda
sasa na kwa sasa tumeomba talaka. Ningetoa taarifa kwa vyombo vya habari hivi
karibuni ili kusema hadithi yangu, si kwa sababu ni haki ya mtu yeyote kujua
kuhusu maisha yangu ya kibinafsi, lakini kwa sababu ninawapenda watu wangu na
ninahitaji wajue kutokuwa na hatia au kosa langu. Endelea kubarikiwa, watu
wangu. Ninawapenda nyote.”
Muda mfupi baadaye, chapisho lingine lilitokea kwenye
akaunti hiyo, likidai kuwa lilikuwa limedukuliwa. "Akaunti yangu ya
Instagram imedukuliwa, juhudi zinafanywa kuchukua udhibiti," chapisho hilo
lilisomeka.