MJASIRIAMALI na staa wa vipindi vya uhalisia kwenye runinga, Zari Hassan amezungumzia mienendo ya uhusiano wake na supastaa wa Tanzania Diamond Platinumz.
Akizungumza siku chache zilizopita baada ya kutua Kenya,
Zari alitoa maelezo ya kile ambacho watu hawajui kuhusu uhusiano wake na
babydaddy huyo wake.
Mama huyo wa watoto 5, wawili kati yao wakiwa wa Diamond
alibainisha kwamba yeye na msanii huyo wa WCB Wasafi wanaendana sana na hilo
halifichiki.
Hata hivyo, alifafanua kuwa ingawa wana uhusiano mzuri,
hautokani na kemia au hisia za kimapenzi.
Zari alieleza kuwa mara nyingi vibe kati yao hukosewa kitu
zaidi ya ilivyo, na kusema kuwa ni matokeo ya wao kushirikiana vizuri kwa ajili
ya watoto wao.
“Bado tunashirikiana vyema katika malezi ya watoto. Mimi na Diamond
tuna jambo hili ambalo tunapokutana, ni vibes nzuri tu, ambayo watu wanakosea
kwa chemistry. Ni vibes nzuri tu kwa sababu sisi sio maadui. Tunalea watoto
wetu pamoja.”
Jibu hili ni tofauti na simulizi iliyoonyeshwa kwenye Young,
Famous & African, ambapo Diamond alidai mara kwa mara kuwa Zari bado ana
hisia naye.
Katika mahojiano hayo, Zari pia aligusia ndoa yake na
Shakib, ambaye alikuwa na wasiwasi kuhusu ukaribu wake na Diamond.
Hapo awali wapenzi hao walikumbana na mvutano kwenye kipindi
hicho Diamond alipopendekeza kuwa Zari bado alitaka kuzaa naye, madai ambayo
Zari aliyakanusha.
Hapo awali Shakib alitilia shaka toleo la mke wake wa matukio
lakini baadaye alimwamini.
Zari alikiri wasiwasi wa mumewe, na kukiri kwamba vibe kati
yake na Diamond wakati mwingine inaweza kuonekana kuwa ya kutatanisha.
Hata hivyo, alieleza wazi kwamba akiwa mwanamke aliyeolewa,
sasa anaelewa umuhimu wa kumheshimu mume wake na ndoa yao.
“Mume wangu ana suala na mimi kuwa karibu na Diamond kwa sababu vibes
ni tofauti, kwa hivyo nikiweza kukata vibe, naelewa sasa kwa sababu nimeolewa.
Nahitaji kumheshimu yeye na ndoa. Kwa hivyo yote hayo ni ya zamani,”
Zari alijirekebisha.