WALIOKUWA wasanii wa injili ambao sasa wanafanya vizuri katika fani ya miziki ya kidunia, Bahati Kioko na Willy Paul wametoa taarifa njema kwa mashabiki wao kuhusu ujio wa kazi zao za kikoa.
Kupitia kurasa zao kwenye mitandao ya kijamii, Willy Paul na
Bahati walichapisha picha wakiigiza picha maarufu ya wanasoka Messi na Ronaldo
wakicheza chess na kufichua kuwa wametoka jikoni tayari kuandaa kolabo
zitakazoashuka kesho Ijumaa.
Pozee alifichua kwamba yeye na Bahati, ambaye tangu
warekebishe urafiki wao Novemba mwaka jana wamekuwa wakirejeleana kama ‘kaka’
wanatarajiwa kutoa kolabo mbili kwa mfululizo kesho.
“Wafalme 2, Nyimbo 2,
Shida Maradufu. Nyimbo Zote Mbili Zinadondoshwa Kesho Saa nne kamili Asubuhi.
Waambie Wasanii Uliowapenda Washikilie Matoleo Yao Kwanza. Tunaiifanya kwa
ajili ya Tasnia ya Muziki ya Kenya... Hebu Turudishe nuru yetu. Videos Kesho Ni
Za Majuu Zote! @bahatikenya Huu Ndio Wakati Bro One Love,” Willy Paul alitamba.
Kwa upande wake, Bahati aliyaradidi maneno ya Willy Paul na
kuwataka makada wake kuwa ange tayari kwa ajili ya mapokezi ya ngoma hizo.
Ukurasa mpya wa mlahaka wa wawili hao ulianza Novemba mwaka
jana pale Pozee alivyoandika barua ya wazi kwa Bahati akimtaka samahani kwa
mambo yote aliyowahi kufanya na kuzorotesha ukaribu wao.
Paul alimtaka Bahati kumsamehe kwa kile alijuta kwamba alikuwa
akivuta majina na picha za familia ya Bahati kwenye mitandao ya kijamii na
kueneza uhasama zaidi.
“Nikikumbuka mambo niliyojionea na kaka yangu, ninatambua
kwamba mara kwa mara nimevuka mipaka. Ninashikilia sana dhana ya familia, haswa
watoto. Matendo yangu hayakukusudiwa kamwe kusababisha madhara, lakini
ninaelewa kwamba yalionekana hivyo, na ninaomba msamaha kwa Diana na watoto Kwa
Upendo wa Kutokuelewana,” Willy Paul aliandika.
Bahati alimjibu akimwambia kwamba mambo ya dunia
hayangewatenganisha huku akikumbuka jinsi walianza safari ya muziki pamoja
miaka ayami nyuma.
“Ndugu Yangu @willy.paul.msafi ,Msamaha Umekubaliwa 🙏 Tumetoka mbali, Sote tumepambana na changamoto nyingi
na umasikini mkubwa katika Vitongoji duni vya Mathare ili kuwa hivi tulivyo leo
na tunapojitahidi kuinuka na kuwa wakuu katika njia tumefanya makosa mengi
lakini cha muhimu ni kurudi nyuma na kurekebisha pale tunapofikiri tulikosea
kwani Mungu wetu ni Mungu wa Upendo na nafasi ya Pili. Zaidi ya yote hakuna
kosa kubwa kuliko udugu tunaoshiriki,” Bahati alisema.