HATIMAYE mmiliki wa kampuni mama ya Facebook, Meta, Mark Zuckerberg amekubali kumaliza kesi ya kumfungia rais wa Marekani, Donald Trump akaunti yake ya Facebook mnamo Januari 2021 kwa kumlipa fidia ya dola milioni 25, sawa na Sh3.23b.
Trump alishtaki kampuni kubwa ya mitandao ya kijamii na
afisa mkuu mtendaji wake, Mark Zuckerberg, mnamo 2021 kwa sababu ya
kusimamishwa kwa akaunti zake baada ya ghasia za 6 Januari Capitol mwaka huo.
Mnamo Julai 2024, Meta iliondoa vizuizi vya mwisho kwenye
akaunti za Facebook na Instagram za Trump kabla ya uchaguzi wa rais wa Merika.
Suluhu hilo liliripotiwa kwanza na Wall Street Journal. Takriban
$22m ya fidia hiyo itaenda kwenye hazina ya maktaba ya urais wa Trump.
Salio litatumika kulipia gharama za kisheria na walalamikaji
wengine waliotia saini kwenye kesi hiyo. Meta haitakubali makosa.
Kampuni hiyo ilisimamisha akaunti za Trump mnamo 2021 na
kusema kwamba ingempiga marufuku kutoka kwa majukwaa kwa angalau miaka miwili.
Baada ya ushindi wa Trump katika uchaguzi wa Novemba,
Zuckerberg alitembelea kituo chake cha mapumziko cha Florida, Mar-a-Lago.
Hatua hiyo ilionekana kama ushahidi wa kurekebika kwa
mahusiano yao ambayo hapo awali yalikuwa ya baridi.
Mwezi uliofuata, Meta ilitoa $1m kwa hazina ya uzinduzi wa
Trump.
Bw Zuckerberg alikuwa mgeni katika hafla ya kuapishwa kwa
Trump katika Ikulu ya Marekani mapema mwezi huu - akiwa ameketi karibu na
mabilionea wengine wa teknolojia duniani.
Kwa miaka mingi, Trump amekuwa akimkosoa sana Bw Zuckerberg
na Facebook - akiita jukwaa hilo "mpinga Trump" mnamo 2017.
Uhusiano wao ulizidi kuzorota baada ya akaunti za rais
kupigwa marufuku. Aliita Facebook "adui wa watu" mnamo Machi 2024.
Twitter, ambayo sasa inaitwa X na inayomilikiwa na mshirika
wa Trump Elon Musk, pia "ilimsimamisha" rais kutoka kwa jukwaa lake.
Baada ya kununua kampuni hiyo kwa $44bn, Bw Musk alirejesha
akaunti ya Trump mnamo 2022 baada ya kura ya maoni aliyoendesha kwenye tovuti hiyo
kuunga mkono hatua hiyo.