logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nilianizana na mume wangu tukilala chini kwenye mkeka - Juma Lokole

Ndoa nzuri ni ile mnajikaza nyote na mnafurahia kila hatua mnayopiga pamoja

image
na Japheth Nyongesa

Burudani31 January 2025 - 09:24

Muhtasari


  • Anatofautiana na wanawake ambao hupendelea kuingi kwenye ndoa wakati kila kitu kiko shwari.
  • Lakini iwapo mali hio wametafuta wote basi mke pia ana mamlaka juu yake.


Mwanadada Juma Lokole ni mwanahabari maarufu katika taifa la Tanzania kwenye Mashamsham, amefichua mwanzo wa maisha yao katika ndoa na mumuwe.

Kulingana na yeye anatofautiana na wanawake ambao hupendelea kuingi kwenye ndoa wakati kila kitu kiko shwari.

Amesistiza kwamba ndoa nzuri ni ile mnajikaza nyote na mnafurahia kila hatua mnayopiga pamoja kuliko kuingilia katikati ya maisha ya mtu pasipokuchangia chochote.

amewataka wanawake wanaoingia kwenye ndoa iliyo na kila kitu kuelewa kwamba mali hio sio yao. mwanaume ana haki ya kuitumia mali hio na wazazi wake sababu ndio walijituma kumusaidia mtoto wao.

Lakini iwapo mali hio wametafuta wote basi mke pia ana mamlaka juu yake.

"Nawaambia watoto wa 2 000, nawapa mfano mimi nilianzana na mume wangu tukilala sakafuni kwenye mkeka. usingoje mtu ana maisha yake kisha ujiingize ndani na uchukue mamlaka.

Mume yule ana wazazi wake wamemsomesha kwa kuuza mifugo na mikopo, heshimu kwa wenyewe ulikopata vimeundwa.

Mvumilivu hula mbivu usingoje mtu kapambana kajenga, mzazi wake amemsomesha anachezea kalamu kisha wewe uwende hapo na starehe zako," alieleza  mwanahabari huyo.

Tena amewataka watoto wa kiume kuwa maakini wanapoingia kwenye ndoa. Kwamba wake zao wasiwe wa kuwafanya kuwachukia wazazi wao.

"Utapata umemuoa mke, ashaanza kukuambia mama yako mbaya, mchawi. kwani wewe kuna kipi hujui kwenu ulikoishi tangu mwanzo ndo uambiwe. Tena kwenye gari kiti cha mbele unakaa na mzazi wako ndo alijikaza na wewe ukafika ulipo," aliongoza Mwanadada huyo.




RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved