logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Namwamba Amhongera Muthoni Kwa Kuweka Rekodi Ya Kukumbatia Mti Kwa Saa 48

“Hongera Muthoni kwa rekodi ya dunia ya kufana ya kukumbatia mti jioni hii katika bustani ya Michuki jijini Nairobi," Namwamba aliandika.

image
na MOSES SAGWEjournalist

Burudani02 February 2025 - 14:45

Muhtasari


  • Muthoni alianza safari ya kuweka rekodi hiyo mpya siku mbili zilizopita ambapo alilenga kuukumbatia mti mmoja kwa saa 48 mfululizo.
  • Rekodi ya awali ilikuwa inashikiliwa na mwanahabari kutoka Ghana kwa jina Hakim Abdul ambaye alikumbatia mti kwa saa 24 mfululizo.

ALIYEKUWA Waziri wa michezo na vijana Ababu Namwamba amemhongera mrembo Muthoni Truphena kwa kuweka rekodi mpya kwenye kitabu cha Guinness ya kukumbatia mti kwa saa 48 mfululizo.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Namwamba aliungana na mrembo huyo mwenye umri wa miaka 21 katika bustani ya Michuki kusherehekea rekodi hiyo.

Muthoni alianza safari ya kuweka rekodi hiyo mpya siku mbili zilizopita ambapo alilenga kuukumbatia mti mmoja kwa saa 48 mfululizo.

Rekodi ya awali ilikuwa inashikiliwa na mwanahabari kutoka Ghana kwa jina Hakim Abdul ambaye alikumbatia mti kwa saa 24 mfululizo.

“Hongera Muthoni kwa rekodi ya dunia ya kufana ya kukumbatia mti jioni hii katika bustani ya Michuki jijini Nairobi. Miguu yako ya kihistoria imevutia usikivu wa kimataifa kwa nguvu ya ajabu ya vijana kuwa mabingwa wa matokeo ya hali ya hewa, uendelevu na kupeleka asili kwa afya ya akili na siha. Roho yako ya Wangari Maathai inatutia moyo sote kusonga mbele na kuifanya dunia kuwa bora, salama, endelevu kwa ajili yetu na kwa vizazi vya huko. Nimefurahi kushuhudia ukiandika historia moja kwa moja. Hongera SHUJAA!” Ababu Namwamba alichapisha kwenye X.

Awali tuliripoti kwamba mrembo huyo mwenye umri wa miaka 21 alikuwa mbioni kuweka rekodi hiyo mpya ambayo alisema nia yake inalenga kutoa ufahamu juu ya umuhimu wa Asili katika kupambana na maswala ya afya ya akili ambayo anayataja kama janga nchini.

Kwa mujibu wa jarida la People Daily wiki iliyopita, Muthoni alifichua kwamba alikuwa amefanya maandalizi kwa ajili ya mchakato wa kuweka rekodi hiyo kwa siku kadhaa.

"Nimekuwa nikitembea kwa muda mrefu kila asubuhi na jioni kwa wastani wa kilomita 42, hii imesaidia katika kuimarisha misuli yangu," aliongeza.

Pia amemshirikisha kocha wa yoga kwa ajili ya kujitayarisha kiakili.

Alikuwa amewaalika Wakenya wote kujitokeza kushuhudia rekodi hiyo ya kihistoria katika bustani ya Michuki.

Bustani ya Michuki, ambayo zamani ilijulikana kama Mazingira Park, iko kando ya Mto Nairobi kutoka Globe Roundabout hadi Daraja la Makumbusho na ina upana wa eneo la takriban hekta 10.4.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved