Milka Moraa, mwanamke aliyeteka hisia za kitaifa baada ya Mchungaji Ng'ang'a kumudhalilisha hadharani kwa madai ya kuomba msaada wa kodi wakati wa ibada kanisani, amejipatia nyumba za bei nafuu ambazo zinajengwa na serikali.
Swala la Milka sasa linaweka wazi masaibu ambayo watu wa tabaka la chini hukumbana nayo hasa wale wanaoishi kwenye vitongoji duni.
Siku chache zilizopita masaibu ya moraa yaligonga vichwa vya habari alipotembelea kanisa la Neno Evangelism Centre mjini Nairobi kutafuta usaidizi wa kulipa kodi ya nyumba.
Moraa aliweka wazi kwamba alikua amefungiwa nyumba baada ya kukosa uwezo wa kulipa kodi ya shilingi elifu nane alizokuwa akidaiwa.
Mchungaji wa kanisa hilo James Ng'ang'a alimufokea mwanamke huyo akimutaka kutafuta usaidizi mahali kwingine akisema hio ilikuwa sehemu ya maombi tu.
"Enda polisi. polisi ya kwenu ni wapi? Sasa umefungiwa nyumba umekuja hapa kutafuta pesa. hapa ni kwa maombi.
Mambo yaliyomkuta Moraa huenda ndio ilikuwa nafasi ya kufungulia baraka zake. Baada ya video hiyo kusambaa mindaoni, afisa wa asikari polisi Sammy Ondimu Ngare kwa kusaidiana na wakenya wenye nia nzuri walichangisha pesa ili kumusaidia mwamnamke huyo kupata makao.
Moraa alianza mchakato wa kupata nyumba katika eneo la makazi ya kijamii ya Mukuru. Kitengo cha kujihifadhi, [Affordable housing]. Nyumba hii imegarimu Ksh640,000, inajumuisha eneo la jikoni, bafuni, na choo.
" Sikuwahi waza kwamba siku kama hii itakuja kutokea katika maisha yangu . Maisha ambayo nilikuwa naishi yalikuwa ya wasiwasi lakini kwa sasa nina matumaini. sasa ninaweza wapa watoto wangu maisha ya baadaye yasiyo na uwoga," alisema Milka Moraa baada ya kupata nyumba.
Kaimu mkurugenzi mtendaji wa nyumba za bei nafuu, Sheila Waweru pia alizungumzia swala hilo nakusema kwamba kufaulu kwa Moraa kunatoa matumaini kwa changamoto ambazo watu hupitia.
Waweru pia aliangazia msaada mkubwa kutoka kwa Wakenya mtandaoni, ambao walikusanya zaidi ya Ksh400,000 ili kuweka depositi ya nyumba. Moraa atatumia mapato yake kulipa hatua kwa hatua rehani iliyobaki.
"Safari ya Moraa ni ukumbusho wenye nguvu na changamoto nyingi zinazowakabili watu, lakini pia ni mfano wa jinsi mpango wa makazi ya bei nafuu inaleta utofauti inavyoonekana" alisema Sheila Waweru.