logo

NOW ON AIR

Listen in Live

RIP! Mtangazaji Mkongwe Leonard Mambo Mbotela afariki

Mwanahabari mkongwe wa Kenya Leonard Mambo Mbotela amefariki dunia.

image
na Samuel Mainajournalist

Burudani07 February 2025 - 11:27

Muhtasari


  • Mwanahabari huyo mkongwe alikuwa hajisikii vizuri kwa muda na alikata roho mwendo wa saa tatu unusu asubuhi siku ya Ijumaa.
  • Mwanahabari huyo nguli alisifika kwa kipindi chake maarufu cha redio na TV kilichoitwa Jee Huuu ni Ungwana.
Leonard Mambo Mbotela

Mwanahabari mkongwe wa Kenya Leonard Mambo Mbotela amefariki dunia.

Mkwe wake Anne Mbotela alithibitisha habari hizo za kusikitisha kwa Radio Jambo Ijumaa asubuhi.

Mwanahabari huyo mkongwe alikuwa hajisikii vizuri kwa muda na alikata roho mwendo wa saa tatu unusu asubuhi siku ya Ijumaa.

"Ni kweli baba mkwe wangu amefariki," Anne alisema.

Mbotela alikuwa amemuoa Alice Mwikali ambao kwa pamoja walipata watoto watatu: Aida Mbotela, Jimmy Mbotela na George Mbotela.

Mwanahabari huyo nguli alisifika kwa kipindi chake maarufu cha redio na TV kilichoitwa Jee Huuu ni Ungwana kilichopeperushwa kwenye redio na TV za KBC.

Programu hiyo iliundwa mnamo 1966 na ilifurahia kupeperushwa kwa takriban miaka 55.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved