
MWANAHABARI nguli wa taarifa za spoti mitandaoni, Fabrizio Romano ameonyesha furaha ya kipekee baada ya gwiji wa soka Lionel Messi kutoa maoni kwenye chapisho lake.
Muitaliano huyo anayefurahia ufuasi wa zaidi ya watu milioni
22 kwenye Facebook alichapisha taarifa kuhusu kinywaji kipya anachokitumia
mwanasoka Lionel Messi na wanatimu wenzake Inter Miami.
“Mas+ ya Lionel Messi
sasa ndicho kinywaji rasmi cha kuongeza maji mwilini cha Inter Miami,” Fabrizio Romano alichapisha
akifuatisha na picha ya Messi akinywa kinywaji hicho uwanjani.
Katika hali nadra zaidi kushuhudiwa, Messi mwenye ufuasi wa zaidi ya watu milioni 117 alifika kwenye chapisho hilo na kutoa maoni yake kwa kutumia emoji za kuinua mikono juu.
Romano ambaye hakuwa anaamini kabisa alipiga screenshot hiyo
na kumshukuru Messi kwa kugundua kwamba anamfuatilia mitandaoni na pia
kushukuru wafuasi wake kwa kufanya ukurasa wake kuwavutia watu maarufu.
“Najivunia ukurasa wangu
wa Facebook na jumuiya. Kuona Leo Messi akija hapa, kusoma chapisho letu na
kutoa maoni… ni wakati mwafaka kwangu,” Romano aliandika.