MSANII Stevo Simple Boy amevunja kimya chake baada ya aliyekuwa mlezi wa wanawe Diana Marua na Bahati, Irene Nekesa kumfungulia moyo kwamba anampenda.
Nekesa katika video moja ambayo ilionekana mitandaoni,
alikiri penzi lake kudondokea kwa msanii huyo ambaye sasa ni mmiliki mpya wa
gari jijini, aina ya Mazda Demio.
Katika video hiyo, Nekesa alijimwaya akimwambia Stevo Simple
Boy kwamba yeye ndiye anayemfaa, haswa baada ya Stevo kutendwa katika mapenzi
kwa mipigo kadhaa.
Nekesa aliweka wazi kwamba alikuwa chini ya shinikizo kwa
penzi la Stevo Simple Boy haswa baada ya kumuona akiwa na gari hilo jipya.
“Acha niseme ukweli, mimi
niko na presha, Stevo Simple Boy amenunua gari na hana bibi. Stevo Simle Boy
nakutafuta, uko wapi? Nipigie simu, mimi sitaki kujua gari hilo linaitwa aje,
ninachokuambia ni kwamba mimi niko single na wewe pia hauna mtu,” Irene Nekesa alisema.
“Nioe angalau ukilia hapo
umepiga magoti nakupangusa machozi. Niko hapa, unataka nikuje nikuoshe miguu,
nikupanguse nikufanyiwe masaji, niko hapa kwa ajili yako, uko wapi?” Nekesa aliongeza
akisisitiza kwamba moyo wake unadunda kwake Simple Boy.
Hata hivyo, Stevo Simple Boy alionekana kutotongozeka na
maneno hayo matamu ya Nekesa akisema kuwa anaelewa vizuri kauli hizo
alizozitaja kama ‘mchezo wa taoni’.
“Mchezo wa taoni tunaujua
vizuri sana,’ Stevo alijibu huku akiambatanisha jibu lake na emoji za
kucheka.
Mapema wiki hii, Stevo Simple Boy alifichua kupokezwa zawadi
ya gari jipya aina ya Mazda Demio kutoka kwa muuzaji mmoja wa magari humu
nchini.
Akitambulisha zawadi yake jipya kwa mashabiki wake mitandaoni,
Stevo Simple Boy alionekana amepiga magoti akisujudu kwa furaha ya kuwa mmiliki
wa gari jijini Nairobi.