
SIKU chache baada ya Zuwena Platnumz kudai kwamba atamkwapua msanii chipukizi wa Kenya, Nexxie na kumpeleka Tanzania ili kumkuza kimuziki, mchekeshaji wa humu nchini, Dj Shiti naye amekariri kwamba kipaji cha msanii huyo ni kikubwa ajabu.
Katika video ambayo inaenezwa mitandaoni, DJ Shiti alirekodi
video akifurahia moja ya ngoma za Nexxie Music na kutabiri kwamba chipukizi
huyo akiendelea kwa kasi hiyo, huenda akawavuruga sana wasanii wakubwa Kenya.
Kwa mujibu wa Shiti, Nexxie Music ana fursa nzuri ya kujikweza
na kuwa uso mpya wa muziki wa Kenya, haswa baada ya wengi wa wasanii tegemezi
kuonekana kulegeza kamba na kupunguza kasi katika kuachia miziki ya kuwakosha
mashabiki wa Kenya.
Shiti alisema kuwa msanii huyo ana sauti nzuri, utunzi mzuri
na wa kipekee ambao unaleta ladha halisi ya Kikenya kwenye masikio ya wapenzi
wa muziki.
“Anaitwa Nexxie Music msanii chipukizi kabisa kutoka +254, huyu anaenda kusumbua sana sanaa ya muziki. Talanta tupu kutoka Kenya. Nexxie hii nimeweka tiki,” Dj Shiti alisema katika video hiyo.
Ungamo la Shiti kuhusu ubora wa chipukizi huyo linajiri
wakati ambapo mrembo aliyepata umaarufu baada ya kucheza kama pambo kwenye
video ya Zuwena ya Diamond Platnumz kuwasuta Wakenya, akisema kuwa wangekuwa
wanajua kuwashika machipukizi wao mikono, basi Nexxie angekuwa miongoni mwa
majina makubwa.
Mrembo huyo alitishia kumchukua Tanzania na kumsimamia
kimuziki huku akiwatahadharisha Wakenya dhidi ya kukurupuka kuwa ni wao wakati
nyota yake itakapong’aa.
“Wakenya wanapenda kuongea sana lakini kupigana support
hawawezi. Kitu kidogo wanapakini, mbona mnapaniki Kenya, mbona? Wakenya mnajua
kuongea sana lakini hamwezi ku’support wenzenu,” alitupa jiwe kwa Wakenya.
“Mimi nataka nimchukue huyu Nexxie nimlete Tanzania
nimsimamie kimuziki ila akijak ufikia kiwango Fulani wasije kudai kwamba ooh ni
msanii wetu wakijibvunia. Hawawezi jivunia kwa sababu mimi nitakuwa
nimembadilisha kuwa wa huku,” aliongeza.
Nexxie Music ni moja kati ya majina ya
ajabu yaliyoteka maskio ya wapenzi wa muziki nchini Kenya tangi mwaka jana.
Msanii huyo kwa sasa anatamba na kibao
chake cha ‘We Hafi Do It’ ambacho kilitoka takribani wiki mbili zilizopita.