
RECHO Elias, maarufu kama Zuwena wa Diamond amewatupia dongo kubwa Wakenya kwa kile anahisi kwamba wana tantarira nyingi sana lakini vitendo sifuri.
Akizungumza kwenye klipu moja, vixen huyo aliyepata umaarufu
miaka miwili iliyopita baada ya kutumika kama mpambe kwenye video ya wimbo wa
Diamond Platnumz ‘Zuwena’ alisema kwamba ana mpango wa kumchukua msanii
chipukizi kutoka Kenya na kumpeleka kwao Tanzania kumsimamia katika masuala ya
kimuziki kwa lengo la kumuinua.
“Wakenya wanapenda
kuongea sana lakini kupigana support hawawezi. Kitu kidogo wanapakini, mbona
mnapaniki Kenya, mbona? Wakenya mnajua kuongea sana lakini hamwezi ku’support
wenzenu,” alitupa jiwe kwa Wakenya.
Zuwena alisema kwamba japo wengi wanahisi Bien ndiye msanii
bora kutoka Kenya – haswa baada ya kushinda tuzo ya Trace kama msanii bora wa
ukanda wa Afrika Mashariki akiwapika wengine kama Diamond, kwake yeye msanii
chipukizi kwa jina Nexxie ndiye msanii bora.
“Sisi Tanzania [kimuziki]
ni wakali sana, lakini Kenya wana mtu wao mmoja tu ambaye mimi namkubali. Ni nanajua
tena anajua sana. Ni msanii mmoja hivi ambaye anaitwa Nexxie, msanii mkali
sana,” Zuwena alisema.
Zuwena alisema kwamba Nexxi Music, japo ni chipukizi lakini
anajua sana sit u kuimba, bali pia kuandikwa nyimbo na hata kwenye kutumbuiza
mubashara.
“Kwanza anajua kuimba,
hata kwenye performance anajua kucheza na steji. Ila sasa wao Wakenya hawawezi
waka support msanii wao wa Kenya. Wanachojua ni maneno mengi.”
Akitangaza mpango wa kumchukua na kumsimamia kimuziki, Zuwena
alitoa onyo kwa wakenya wasije wakaanza kudai kwamba Nexxi ni wao baada yake
yeye kumpaisha ngazi kumuziki.
“Mimi nataka nimchukue huyu Nexxie nimlete Tanzania nimsimamie kimuziki ila akijak ufikia kiwango Fulani wasije kudai kwamba ooh ni msanii wetu wakijibvunia. Hawawezi jivunia kwa sababu mimi nitakuwa nimembadilisha kuwa wa huku,” aliongeza.
Nexxie Music ni moja kati ya majina ya ajabu yaliyoteka
maskio ya wapenzi wa muziki nchini Kenya tangi mwaka jana.
Msanii huyo kwa sasa anatamba na kibao chake cha ‘We Hafi Do
It’ ambacho kilitoka takribani wiki mbili zilizopita.
Msanii huyo amefanya ngoma kadhaa ikiwemo kolabo na mkali wa
Dancehall, Redan – kibao kwa jina Vile Inafaa lakini pia ana ngoma zake
mwenyewe kama Far, Hela, We Gide More, Shake Up miongoni mwa nyingine.