
SOSHOLAITI na mfanyibiashara wa Uganda mwenye makao yake Afrika Kusini, Zari Hassan amezungumzia kauli aliyoitoa Diamond Platnumz kwenye kipindi cha uhalisia cha Netflix kwamba mama huyo wa Watoto 5 anaweza mrudia wakati wowote.
Akizungumza pindi alipotua nchini Kenya,
Zari aliitaja kauli hiyo ya babydaddy wake kama ubinafsi wa hali ya juu, akionekana
kuikanusha.
Zari alisema kwamba kwa upande wake haoni
kama Diamond ana kile kinachohitajika ili kumrudisha kwake, kinyume na jinsi
Diamond alidai kwamba Zari anatamani kumrudia.
"Diamond anasema chochote
anachojisikia kwa sababu inalisha ubinafsi wake. Diamond ana ubinafsi, na unahitaji
kulishwa kila wakati. Lakini sio juu ya kile anachosema - je, ninafanya hivyo?
Je, ni kweli kwamba anaweza kumrudisha tena Zari?” Zari alisema.
Hata hivyo, Zari alisema kwamba yeye hana
tatizo na Diamond kwani mwisho wa siku anasalia kuwa baba kwa wanawe wawili na
hawezi badilisha uhalisia huo.
Mjasiriamali huyo alisema kwamba kwa
kipindi ambacho amemjua Diamond, anamuelewa kwamba ni mtu mwenye majivuno na
ubinafsi mwingi, hivyo akimsikia akitoa kauli ya kujigamba, yeye anajua fika
kwamba huo ni ubinafsi wake unazungumza na hawezi kuchukia.
"Kwa hivyo kwangu, mimi ni kama, nah,
hiyo ni ego yako tu, na niko sawa na hilo."
Kauli yake inajiri wiki kadhaa baada ya
Diamond katika sehemu yake kwenye kipindi cha Young Famous and African kwenye
Netflix alisema kwamba yeye ako na kila kinachohitajika kumrudisha Zari kwake.
Katika mahojiano hayo, Diamond alikariri
kwamba Zari hawezi kataa ombi la kurudi kwake ikiwa angelipendekezewa, akiashiria
kwamba Zari bado ana hisia za mapenzi kwake.
Hii ni licha ya kila mmoja kusonga mbele na
maisha yake, Diamond sasa akiwa katika uhusiano na msanii wa lebo yake, Zuchu
huku Zari akifunga ndoa ya Nikkah na mpenzi wake Shakib Cham Lutaaya.
Kulingana naye, ziara yake nchini Kenya
inahusiana kabisa na biashara, na ana miradi kadhaa iliyopangwa.