logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Zari atishia kupata mume mpya huku Shakib akikabiliwa na madai ya kumsaliti kimapenzi

"Wanaume wanaweza kukuacha jangwani bila maji. Msishangae nikikutambulishia mkwe mpya," Zari alisema.

image
na Samuel Mainajournalist

Dakia-udaku06 March 2025 - 08:26

Muhtasari


  • Shakib amekanusha vikali madai hayo, akisisitiza kuwa video hiyo si ya sasa na inalenga kumharibia jina pamoja na kuvuruga ndoa yake.
  • Zari ameonekana kuashiria kuwa anaweza kuachana na Shakib iwapo ataendelea kusikia habari za usaliti.

Zari Hassan with Shakib Cham

Mfanyabiashara wa Uganda, Shakib Cham Lutaaya, amejitokeza na kujibu tuhuma za kumsaliti mke wake, Zari Hassan, baada ya video inayodaiwa kumwonyesha akiwa na mwanamke mwingine kusambaa mitandaoni.

Video ambayo imekuwa ikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii imezua gumzo kubwa, huku wengi wakidai kuwa ni ushahidi wa usaliti wake.

Kupitia akaunti yake ya Snapchat, Shakib amekanusha vikali madai hayo, akisisitiza kuwa video hiyo si ya sasa na inalenga kumharibia jina pamoja na kuvuruga ndoa yake.

"Tafadhali puuzeni video hiyo inayosambaa, ni ya zamani," alisema Shakib.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 33 aliongeza kuwa watu wanaoeneza video hiyo wanajaribu kumchafulia jina na kuleta mgogoro katika mahusiano yake na Zari.

"Hii ni njama ya bloga anayepania kuchafua jina langu na kuvuruga mahusiano yangu," alisisitiza.

Kwa upande wake, Zari Hassan hakusalia kimya. Kupitia video aliyochapisha kwenye mitandao ya kijamii, aliandika ujumbe ulioeleza hisia zake kuhusu madai hayo.

"Wanaume wanaweza kukuacha jangwani bila maji. Msishangae nikikutambulishia mkwe mpya," aliandika, akionekana kuashiria kuwa anaweza kuachana na Shakib iwapo ataendelea kusikia habari za usaliti.

Licha ya hali hiyo, Zari alieleza kuwa kwa sasa anaweka mkazo zaidi kwenye ibada ya mwezi mtukufu wa Ramadhani na hataki kuvurugwa na drama za mitandaoni.

Hii si mara ya kwanza kwa mahusiano ya Shakib na Zari kuandamwa na tuhuma za usaliti. Tangu walipoanza mahusiano yao mwaka 2022, wamepitia changamoto kadhaa ambazo zimeacha mashabiki wao wakiwa na maswali mengi.

Mwaka wa 2023, ziliripotiwa habari kwamba Shakib alikuwa bado kwenye ndoa na mwanamke mwingine wakati alipokuwa akichumbiana na Zari.

Hata hivyo, alikanusha vikali madai hayo. Pia, ndoa yao ya kitamaduni ilizua mijadala, huku baadhi ya watu wakimshutumu Zari kwa kuchagua mwanaume "asiye na hadhi" wakimlinganisha na aliyekuwa mpenzi wake, Diamond Platnumz.

Licha ya drama hizi, wawili hao wamekuwa wakionekana pamoja mara kwa mara, wakionesha kuwa bado wanashikilia ndoa yao. Hata hivyo, kauli ya hivi karibuni ya Zari imeibua maswali kuhusu mustakabali wa uhusiano wao.

Wakati mashabiki wao wakiendelea kujadili, bado haijulikani ikiwa Zari atasimama na mumewe au atasonga mbele kama alivyodokeza.


Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved