Zari kwenye mahojiano na mwanahabari amesema kwamba ni ukweli na hata watu wa Tanzania wanafahamu hilo. Mwanadada huyo alifichua hayo na kueleza kwamba siyo yeye peke aliyemwambia Fantana hata wasani wengine wa kike walimufichulia.
"Nilimwambia kwani ni uwongo, mpaka kina Nadia wamemwambia kitu hicho hicho, Kanye amemwambia, kuna dada mwingine hapo Rozeti amemwambia kweli Diamond ana mtu kule," alifichua Zari.
Mwanamziku huyo tokea Uganda amesisitiza kwamba kumwambia Fantana kuhusu mahusiano ya Diamond si wivu maana kwa sasa hata yeye ana mtu wake.
"Nyinyi ni wa Tanzania kwani nilisema uwongo? ..Yaani acha nikwambia kabisa hainihusu sasa hivi. Mimi kukuambia hivyo haimaanishi chochote, sai mimi naangalia kuwa mwanamke tofauti wa baadaye. Sasa mimi imeonekana ni kama nina wivu, mimi namwambia sina shida 'Diamond' yuko na mtu wake na mimi nina mtu wangu," alisema Zari.
Mwanamziki Zari na nyota wa bongo fleva Tanzania Diamond Platinumz waliwahi kuwa kwenye mahusiano ya mapenzi kwa muda mrefu. Wawili hao wana watoto wawili ambao wamezaa pamoja.
Baada ya mahusiano kati ya Diamond na Zari kuvunjika, Zari aliolewa na Shakib Lutaaya ambaye ni mwanabiashara nchini Uganda.
Zari na Fantana hawaonani macho kwa macho. Mwanadada Zari aliwahi kukiri kwamba hana chuki juu ya Fantana na Diamond kuwa kwenye mahusiano ila aliudhika na vitendo vyao vya kumuongelelea hadharani.
Sikuwa na wivu na yule binti, shida yangu ni kwa baba ya mtoto wangu Diamond, amekaa na mwanamke mwingine akinijadili, namheshimu Diamond sana, yeye ni baba wa watoto wangu na siku zote tutakuwa na uhusiano huu, lakini ukikaa na kunijadili na kumpa mtu mwingine ujasiri wa kuninyanyasa hapo ndipo unapovuka mpaka, "Zari alisema.
"Siwezi kukaa na mume wangu sasa hivi na kuanza kumjadili Diamond, kamwe. Diamond angeweza tu kumtongoza msichana huyu bila kutumia jina langu na najua inawezekana,' alisema Zari awali.