Shakib Cham ameamua kufunguka wazi na kuomba msamaha kwa mkewe Zari baada ya Zari kudai kwamba ameota ndoto mumewe akifunga ndoa na mke mwingine.
Shakib Cham Lutaaya ni mjasiriamali maarufu wa Uganda. Alipata umaarufu kupitia uhusiano wake na Zari Hassan, mshawishi mashuhuri na mfanyabiashara katika mitandao ya kijamii.
Shakib mzaliwa wa Kampala, Uganda, mwenye umri wa miaka 33 aliwashangaza wafwasi wao baada ya kuomba msamaha kwa sababu ya ndoto.
Shakib amemuomba radhi Zari kwa kumuoa mwanamke mwingine. Katika video hiyo amayo imesambasa, Shakib aliomba hadharani msamaha wake kwa Zari.
"Nataka kuomba msamaha kwa Zari kwa kuoa mwanamke mwingine katika ndoto zake," alisema.
Katika video hiyo, Shakib alionesha kujutia kwa kosa alilofanya katika ndoto ya mke wake.
Aidha, aliomba msamaha kwa kutomnunulia chochote alipofika nyumbani.
"Nataka kuomba msamaha kwa mke wangu, nilipompigia simu kumuuliza kama anataka kitu na akasema hataki chochote, nilipaswa kumnunulia kitu," alisema.
Shakib aliamua kuomba msamaha katika mtandao wa TikTok, mbele ya Zari, kwani zari alikubali kwa utulivu msamaha wake.
Watu hao mashuhuri walichukua muda wao kutoa burudani kwa mashabiki wao kupitia kwenye mtandao wa Tiktok.
Mashabiki wa Shakib na Zari walifurahia video hiyo, hata hivyo, wengine waliwaonya kwamba wanapaswa kuwa waangalifu kwamba jambo hilo lisije likaw ukweli kwao siku zijazo.
Zari na Shakib walifanya harusi yao ya kizungu Oktoba 2023. Harusi ya kupendeza ilikuwa mazungumzo ya mji kwa siku kadhaa.
Harusi yao ilikuja miezi kadhaa baada ya kufanya harusi yao ya kitamaduni ya Kiislamu (nikah) huko Pretoria, Afrika Kusini, Aprili 16, 2023.
Zari aliolewa kwa Shakib akiwa na watoto kadhaa, wili miongoni mwao wakiwa wa Bosi wa Wasafi Diamond Platinumz kutokana na kukiri kwake.