logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Diamond alinitongoza nikiwa bado shule - Hamisa Mobetto afichua

Mobeto ameweka wazi kuhusu mahusiano yake na aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Diamond.

image
na Japheth Nyongesa

Mastaa wako18 March 2025 - 08:39

Muhtasari


  • Mobetto kwenye uhusiano na mwanamuziki Diamond Platnumz walimkaribisha mtoto wa kiume, Deedalayan Abdul Naseeb, mwaka 2017.
  • Wanandoa hao baadaye walitengana kwa sababu zisizojulikana.

Diamond platinumz and Hamisa Mobetto
Hamisa Hassan Mobetto  ni mwimbaji wa Tanzania, mwigizaji, mfanyabiashara na mwanajamii ambaye amakuza umaarufu nchini Tanzania na mataifa ya Afrika Mashariki.

Mobeto ameweka wazi kuhusu mahusiano yake na aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Diamond Platinumz ambaye pia ni mwanamziki.

Mwanadada huyo amefichua kwamba Diamond alinza kumutongoza wakati yupo shule na alikuwa angali mwanafunzi.

"Nilimujua Diamond kitambo wakati ningali shule. Nilikutana na yeye sehemu, alikuwa na rafiki yake na hapo ilikuwa kabla hajatokea kimuziki. Mwanzo hakujua kama mimi mtoto nilikua kati ya kidato cha pili na tatu. Aliniomba namba ya simu na nikamwambia sina simu na kiukweli sikuwa na simu siku hizo," alisema Mobetto.

Ikaja kutokea tena mwaka mmoja baadaye nikaja kukutana na yeye tena sehemu ingine. Akaniomba niwe kwa video yake ndio alikua anataka kuanza kuimba na nikamwambia siwezi maana bado niko shule. Akasema kwani una umri wa miaka mingapi, Hapo nilikuwa kati ya miaka 16, 17 hapo," alieleza zaidi.

Mobeto pia aliweka wazi kwamba mahusano yake na Diamond yalianza baada ya msani huyo wa Wasafi kuanza kutoa nyimbo. Lakini pia alifichuwa kwamba walikuja wakapoteleana kwa muda mrefu kidogo kabla ya kukutana tena.

Baadaye 'Diamond' akaja kutoa nyimbo, nikaja kumupenda, nyimbo nzuri lakini sikumuona tena mpaka nilipomaliza kidato cha nne. Baada ya kumaliza shule tukaja kuonana tena. Baada ya kukutana tena tukawa tu marafiki wa kawaida kwa muda lakini sio wapenzi," alisema.

Sasa baadaye ndio nikaja kwenda miss Tanzania na tukaingia kwenye mapenzi baada ya muda tukaachana tena tukarudiana, tukaachana tena,'" mwanadada huyo alieleza.

Kulingana na yeye baadhi ya mambo ya mambo ambayo yalichangia sana mapenzi yao kuwa ya kuyumbayumba mara kwa mara ni kutokana na mahusiano ya Diamond na wanadada wengine jambo ambalo aliliona gumu sana hasa kutokana na umuri wake ambao kiasi ulikuwa bado mdogo.

Unajua yule anapenda wasichana wazuri, nilikuwa naona kama tu hajatulia, alafu mimi nilikuwa mdogo. Ukiiwa na ndoto kisha uko na mtu ambaye anapenda wasichana maarufu na umaarufu kidogo unaogopa maana unaeza ukaharibu kitu," aliweka wazi.

Awali Mobetto alikuwa katika uhusiano na Francis Ciza na wakawa wazazi wa binti, Fantasy Majizzo.Baadaye alikuwa katika uhusiano na mwanamuziki Diamond Platnumz na walimkaribisha mtoto wa kiume, Deedalayan Abdul Naseeb, mwaka 2017. Wanandoa hao baadaye walitengana kwa sababu zisizojulikana.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved