Mshawishi maarufu nchini Tanzania Mwijaku sasa anamtaka mwanamuziki tajika nchi humo Mbosso Khan kutengana na bosi wa Wasafi kwa kile anachotaja kwamba sasa ni wakati wa kushindana maana tayari ameshatoka wasafi.
Mwijaku anaeleza kwamba Mbosso ana uwezo wa kufanya vitu vikubwa akimtaka kuonyesha uwezo wake sasa kibinasi. Vilevile amesema kwamba wakati akiwa Wasafi fedha zake zilikuwa zinakwenda kwenye lebo, lakini sasa ni wakati wa kufanya shuguli zake.
Mwanahabari huyo pia amemuomba Mbosso kufanya kolabo na Aslay akiamini kwamba itakua kali na itakwenda mbali na kuwasongesha katika hatua nyingine kimuziki.
"Mbosso nimushauri akitoka, sasa hivi si ametoka, aache mazoea na Diamond. sasa ni mapambano kwa mapambano. Ameona changamoto alizopitia. yaani Mbosso akiomba kufanya eventi, eventi zinaenda kwa bi Zuhura tu. Alichokifanya Mario, Mbosso kakiomba kwa miezi sita," alieleza Mwijaku.
"Sasa hivi tunakwenda kumuona Mbosso wa ukweli na Mnosso nimushauri sasa hivi tafuta Aslay muekeni kolabo," alikamilisha mtangazaji huyo huku akionesha imani kwamba weakati wa Mbosso kung'aa ni sasa hivi.
Mbosso ni mmoja kati ya wasanii wanaofanya vizuri sana kwenye miziki ya bongo sio tu Tanzani bali Afrika mashariki na mataifa ambayo yanakielewa kiswahili.
Mwanamziki huyo ambaye ni mzoefu wa kuimba Mashari ameachilia vibao kadha huu mwaka ambavyo vinafanya vizuri sana, kikiwemo kibao ambacho kinaitwa 'BODA' ambacho wamekiimba kwa ushirikiano na Billnass pamoja na kibao chake kipya cha "Penzi ni Hadithi'
Mbosso alitangaza kuondoka wasafi mwezi jana na maneno hayo kuthibitishwa na kiongozi wa Wasafi Diamond Platinumz. Mbosso pia alikiri kwamba wakati wa kuondoka kwake hakulipa chochote kwa lebo kutokana na heshima yake alipokuwa huko.
Msani Mbosso hivi karibuni alieleza kwamba licha ya kwamba ametoka Wasafi kimukataba bado wana urafiki mkubwa na Diamond, pia akiongeza kwamba bado wanashirikiana kwa vitu kadha likiwemo la kuichezea timu ya Wasafi katika mpira wa kandanda.