logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanadada wa Kenya afichua kumukufia Diamond Platinumz

Mwanadada wa chuo kikuu hapa nchini Kenya amefichua kwamba anampenda mwanamziki wa Tanzania Diamond Platinimz.

image
na Japheth Nyongesa

Dakia-udaku14 March 2025 - 13:33

Muhtasari


  • Ameendelea na kusema kwamba mwanaume kama Diamond ndiyo tamaa ya moyo wake kwamba siku moja aje kupata nafasi kama hiyo.
  • Diamond amepata wafuasi wengi Afrika Mashariki na Kati.
Diamond Platnumz

Mwanadada wa chuo kikuu hapa nchini Kenya amefichua kwamba anampenda mwanamziki wa Tanzania Diamond Platinimz kwa dhati na akifaulu siku moja kuwa kwenye Mahusiano na yeye hawezi kuiacha nafasi hio kabisa.

Ameendelea na kusema kwamba mwanaume kama Diamond ndiyo tamaa ya moyo wake kwamba siku moja aje kupata nafasi kama hiyo.

"Diamond tu, namucrashia sana. Ananikosesha... simuogopi mtu ata Zuchu, heri tushare wote," alisema mwanadada huyo. Pia alieleza kwamba anaupenda sana muziki wake.

Mrembo huyo alisistiza kwamba kitendo cha Diamond kuwa na wanawake wengi katika mahusino ni jambo la kawaida na huo ndo kuonesha uanaume.

'Napenda sana muziki wake, hunifurahisha sana. Kwa hilo la kuwapenda wasichana wengi, hio sasa ndio kuwa mwanaume. na naweza kuwa naye kujifurahisha," alisema.

Hata hivyo mwanadada huyo amekiri kwamba hakuna kitu chochote dunianiani ambacho kinaweza kumfanya mwanaume asiondoke kwenye mapenzi na kwenda kwingine. Amesisitiza kwamba yule ambaye ni wa kwenda ataondoka tu hata chochote kifanyike.

"Hapa Kenya tunasema wa Kwenda ataenda tu ata ufanye nini. Kama alikuwa aende ataenda ata umueke aje, umufunge Nyumbani wa Kwenda ataenda,' alisisitiza.

Diamond Platnumz, ni msanii wa muziki wa bongo flava nchini Tanzania, mcheza densi, mhisani na mfanyabiashara. Ndiye mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa lebo ya WCB Wasafi , Wasafi Bet na Wasafi Media.

Diamond amepata wafuasi wengi Afrika Mashariki na Kati. Alikuwa msanii wa kwanza wa Afrika kufikia maoni milioni 900 kwenye YouTube.

Diamond ni mwanamziki ambaye anapendwa sana na watoto wa kike na amewahi toka kimapenza na watoto wa kike nchini Tanzania na hata nje ya nchi akiwemo Wema Sepetu, Zari Hasani, Hamisa Mobeto, Tanasha Dona miongoni mwa wengine.

Kwa sasa Diamond yuko kwenye Mahusiano na mwanamuziki ambaye pia yupo kwenye lebo yake ya Wasafi Zuhura Othman Soud maarufu Zuchu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved