Msanii Nasibu Abdul Juma Issack alimaarufu Diamond ameashiria dalili za kumsajili msanii mpya Katika lebo ya WASAFI baada ya Mbosso kuondoka.
Msanii huyo wa Tanzania alitangaza mkataba wa makubaliano kati ya kampuni yake na mwimbaji mpya akiashiria kipaji kingine kipya chaja aliandika katika ukurasa wake wa Instagramu pasi kumtaja jina msanii huyo.
‘’Mkataba wa kujiunga na kampuni ya muziki. Mkataba huu unaingiwa leo terehe 18 mwezi 03, 2025,”Diamond alisema.
Hio ilikuwa ishara tosha kuwa Diamond alikuwa mbioni kumsakama na kumpata nyota mwingine wa muziki ambaye atazidi kutamba na kutaratamba katika Nyanja na katika sanaa hiyo ya kimziki.
Kwa kuzungumzia kuondoka kwake Msanii Mbosso Diamond aliweza kusema kuwa urafiki wao na Mbosso ulikuwa wa viwango vikubwa hata kufikia uamuzi wa kuondoka kwake.
‘’Mbosso wiki mbili na nusu nyuma tumeongea na Mbosso na aliniomba aweze kujisimamia na nikampa baraka zangu zote."
Mbosso ni mdogo wangu nikamwambia Mbosso tumeishi vizuri na hatujawai gombana na wala hatujawai kwazana na kwa jinsi ulivyo niheshimu kwa kunipenda na tukapendana siwezi kukutoza hata shilingi na sijamtoza hata shilingi kumi,” Diamond alifafanua katika mahojianao na kituo kimoja cha habari.
Msanii Diamond alizidi kumsifia na kumwita Mbosso kama rafiki yake tena wa dhati katika masuala mbalimbali ya Kisanaa na kwa kushirikiana jambo ambalo lilisababisha kutomtoza hata senti moja alipotaka kuondoka.
‘’Kwanza ninamshukuru kwa kutumia hekima. Unajua ni wasani wachachwe wanaweza kutumia hekima hiyo kwa sababu kwanza alivyokuja Mbosso alikuwa amekuja kulipa lakini nikwamwambia, bro, tumeishi vizuri nawe na kwa heshima uliyonipa siwezi nikakutoza chochote. Namna nilivyoishi na Mbosso, kumtoza hela ni aibu kwangu. Angekuwepo mtu mwingine ambaye hatujaheshimiana hela unatoa,” alisema.
Hata hivyo kinachosubiriwa kwa sasa na washabiki wa Diamond ni kumuona msanii huyo ambaye wana uchu na ari kuu ya kumuona na kumuweka kwenye mizani ya Wasafi iwapo ataafikia viwango vyake.