
Mbunge Mumias mashariki Peter Salasya amezungumza hadhani kwa wanahabari tangu aliposhambuliwa na baadhi ya mashabiki wa soka katika uwanja wa Nyayo wakati kenya ikichuana na Gabon.
Salasya alitaja kitendo alichofanyiwa kama ambacho kimepitwa na wakati katika taifa la Kenya. Wakati huo amedai kwamba tukio hilo lilipangwa na wanasiasa maarufu nchini.
"Sijazungumzia hili hadharani kwa wanahabari, lakini nimefikia Gen Z kwa mitandao yetu maana iko na wafwasi wengi. Mwanzo kabisa nataka kulaani vikali kile kilitokea. Peter Salasya hafai kuchukuliwa kama mtu ambaye hana umuhimu. Mimi ni mtu mkubwa kwa nchi, na nafaa kuchukuliwa kuwa miongoni mwa wanasiasa 10 maarufui nchini," alieleza.
Mbunge huyo alidai kwamba waliompiga ni wafwasi wa ODM,wakora na watu wa Raila. Ameeleza kwamba alianza kupewa msomo tu wakati aliwasili kwenye lango kuu la kuingia uwanjani na kuwataja watu ambao walipewa jukumu la kumuelekeza akiwa uwanjani walihusika kumpiga.
'Nataka kuwaambia wafwasi wa ODM, mimi nilienda kutizama mpira na sikujua kama furugu zitatokea. nilijua mpira unaleta wakenya pamoja na nilikuwa huko. Na nashangazwa kweamba walipigwa kwa sababu walifukuza baraka," alisema
"Kufika tu kwa gate watu walianza kunipea warning, wengine walikuwa wamevaa jackets za FKF na walihusia kunipiga na kunifukuza,'alieleza zaidi.
Mwanasiasa huyo alisisitiza kwamba Raila ni mtapeli wa siasa na hawezi kuomba msamaha kwani alichokisema ni ukweli.
'Raila aliposema tumerudi mimi nikauliza tumerudi wapi, yeye ni mtapeli wa siasa na mnajua amekuwa kwa serikali tatu. Alikuwa kwa saerikali ya kibaki, alikuwa kwa serikali ya Uhuru na yuko kwa serikali ya Ruto," Salasya alisema.
"Siwezi omba msamaha kwa kuita Raila mtapeli wa siasa, sababu mimi nilikuwa kwa maandamano ya sufuria, akishafanikiwa anaenda pekee yake bila kutuuliza huo si ni utapeli wa siasa," aliweka wazi.