
ALIYEKUWA mama wa kaunti ya Machakos Lillian Nganga ametilia shaka viwango vya elimu humu nchini, akihoji ni vipi Kenya ilijipata katika nafasi ya kuwa na watu wengi wenye uwezo wa kuandikwa na kusoma lakini hawajui kujieleza vizuri.
Kupitia ukurasa wake wa X, bi Nganga alidai kwamba vijana
wengi nchini ni wasomi lakini wachache ndio wanajua kuandikwa na kujieleza
vizuri.
“Inakuwaje kiwango cha
watu wa Kenya kujua kusoma ni kikubwa, ilhali vijana wengi hawawezi kuandika na
kujieleza vizuri?”
Mama huyo wa mtoto mmoja wa kiume aliyepata na rapa Juliani
alisema kwamba tatizo hilo aghalabu lilianza baada ya kizazi cha Millenials.
Kulingana na Nganga, inashangaza sana kuona mabadiliko hayo
makubwa ya kwamba watu wengi ni wasomi wasioweza kujieleza licha ya kutokuwa na
mabadiliko makubwa ya utoaji wa elimu kati ya kizazi cha Millenials na Gen Z.
“Nadhani kupungua
kulianza baada yetu (milenia), kwa hivyo nashangaa ni nini kilibadilika kwani
msingi wa mfumo wa elimu haujabadilika kiasi hicho!” alihoji.
Nganga katika siku za hivi karibuni ameonekana kuzamia zaidi
masuala ya siasa, akitoa maoni yake kuhusu siasa za Kenya bila kubabaishwa na
mashambulizi kutoka kwa baadhi ya watumizi wa mitandao ya kijamii.
Wiki chache zilizopita baada ya kuweka wazi kwa mara ya
kwanza kwamba penzi lake na Juliani lilikuwa limegonga mwamba, na akaweka wazi
kuwa katika maisha yake tangu atomize miaka 25 hadi sasa anapokaribia kufikisha
miaka 40, amekuwa na wanaume 2 tu.
“Je, ukweli kwamba
nimekuwa na wanaume wawili tu tangu nikiwa na umri wa miaka 25 (ninatimiza
miaka 40 mwaka huu) unawezaje kunifanya mambo yote ya kipuuzi mnayoniita? 🤣 Pumbavu, Wajinga sana!” Lillian Nganga alichapisha.
Akirejelea uhusiano wa zaidi ya miaka 10 na aliyekuwa
gavana wa Machakos ambaye sasa ni Waziri wa leba Alfred Mutua ambao ulivunjika
mwaka 2021, Nganga alisema kwamba anajionea Fahari kuwa miongoni mwa watu
waliosimama na mwanasiasa huyo katika kampeni mara mbili na kushinda ugavana
naye.
Nganga aliyeonekana
kusimama kidete pasi na kutetereka dhidi ya mashambulizi kutoka kwa
wanamitandao alisema kwamba huo ni mwanzo tu na yeyote ambaye atashindwa
kustahimili majibu yake basi ajiondoe mapema kwenye gumzo.